CURRENT NEWS

Saturday, February 24, 2018

MAMA SAMIA AWATAKA SKAUTI NCHINI KUSHIRIKI KATIKA SHUGHULI ZA UZALISHAJI MALI KUJIONGEZEA KIPATO

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akifungua mkutano mkuu wa Skauti Tanzania.

 Washiriki wa mkutano.
 Washiriki wa mkutano.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akisalimiana na Mdhamini wa Skauti Tanzania,Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Mhe.Ali Hassan Mwinyi.
 Makamu wa Rais wa Skauti Tanzania Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry akizungumza kwenye mkutano mkuu wa Skauti.
 Skauti Mkuu Mama Mwantumu Mahiza akizungumza kwenye mkutano mkuu wa Skauti.
.........................................................
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan amewataka Skauti nchini Tanzania kushiriki katika shughuli za Uzalishaji mali kwa lengo la kujiongezea kipato na kukabiliana na changamoto ya Ukosefu wa Ajira hasa kwa Vijana.

Hayo yamesemwa leo Mkoani Dodoma katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Skauti Nchini uliofanyika katika Ukumbi wa Pius Msekwa ambapo Hotuba ya Makamu wa Rais ilisomwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde ambaye ndiye alikuwa Mgeni Rasmi katika mkutano huo uliohudhuriwa pia na Mdhamini wa Skauti Tanzania,Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Mhe.Ali Hassan Mwinyi.

Katika hotuba hiyo,Makamu wa Rais  amewapongeza skauti kwa kushiriki katika matukio ya kijamii ikiwemo wakati wa maafa Kilosa na Pugu kwenye machimbo.

Aidha amewataka skauti kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba Amani na Mshikamano wa nchi unalindwa kwa nguvu zote.

Awali akimkaribisha Mgeni Rasmi, Makamu wa Rais wa Skauti Tanzania Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry amebainisha mipango mbalimbali ya Skauti Tanzania katika kujiletea maendeleo na pia amemhakikishia Mgeni Rasmi kwamba Skauti Tanzania itaendelea kujikita katika kusimamia HAKI,USAWA na UZALENDO pamoja na kuhimiza AMANI na  MSHIKAMANO miongoni mwa Watanzania.

Mkutano huu Mkuu wa Skauti agenda yake kuu ni Uchaguzi wa Uongozi wa Skauti na Wajumbe wa Bodi.
Kwasasa sasa Skauti Tanzania ipo chini ya Uongozi wa Skauti Mkuu Mama Mwantumu Mahiza na Kamishna Mkuu Abdulkarim Esmail Shah.


 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania