CURRENT NEWS

Tuesday, February 27, 2018

MIRADI YA MAENDELEO KUFANYIWA MAPITIO YA KIMKAKATI


 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo

akifungua Kikao kazi cha kujadili mpango wa utekelezaji wa miradi ya inayotekelezwa
kwa Fedha za mfuko wa Maendeleo ya Serikali za Mitaa.
 Katibu Mkuu OR-TAMISEMI Mhandisi Mussa Iyombe akizungumza na wajumbe wa

Kikao Kazi(hawapo pichani) kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua Kikao
hicho.
 Katibu Mkuu OR-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Dkt.Laurean

Ndumbaro akizungumza na wajumbe wa Kikao Kazi cha kujadili mpango wa
Utekelezajo wa Miradi ya LGDG.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo

(Mbele aliyesimama) akizungumza na wajumbe wa Kikao kazi cha kujadili mpango
wa utekelezaji wa miradi ya LDGD
 Baadhi ya Wakurugenzi wa OR-TAMISEMI wakibadilishana mawazo wakati wa Kikao

kazi cha kujadili utekelezaji wa Miradi ya LGDG.
Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Wakili Kiomoni Kiburwa Kibamba

akiwa na Mchumi wa Jiji wakifuatilia Kikao kazi cha kujadili Utekelezaji wa Miradi ya
LGDG kilichofanyika Chuo cha Mipango Dodoma.
.........................................................................................................
NTEGHENJWA HOSSEAH, OR-TAMISEMI.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo
amewataka viongozi wa Halmashauri zote Nchini kupitia mipango iliyopo (Review) na
kupanga Upya Kimakati miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa kwa Fedha za mfuko wa
Maendeleo ya Serikali Mitaa (LGDG).

Waziri Jafo ameyasema hayo kwenye Kikao Kazi cha kujadili Mpango wa Utekelezaji wa
Miradi ya LGDG iliyoboreshwa kwa mwaka wa Fedha 2017/2018 kilichohusisha baadhi ya
Wah. Wabunge, Mameya, Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali
za Mitaa pamoja na Maafisa Mipango kilichofanyika katika chuo cha Mipango kilichopo mjini
Dodoma.

Waziri Jafo alisema kuwa Bajeti ya Mfuko wa Maendeleo ya Serikali za Mitaa kwa mwaka
huu wa Fedha ni Bil.251 ambazo hugawanywa kwa halmashauri zote Nchini. Fedha hizi ni
nyingi sana na zinatosha kutekeleza miradi michache yenye Tija na itakayopunguza
changamoto kwa wananchi wetu lakini kinachofanyika ni kuwa halmashauri hugawanya
kiasi wanachopata kwenye miradi mingi ambapo sio rahisi kuona matokeo kwakuwa miradi
mingi haikamiliki.

“Katika Halmashauri nyingi badala ya kugawanya Fedha hizi za Ruzuku kwenye miradi mingi
kwa viwango kidogo kidogo ni vyema sasa tukajieleza kwenye miradi michahe ambayo
tutahakikisha inakamilika kwa mwaka wa Fedha husika na kuanza kutoa huduma kwa jamii”
Alisema Jafo.

“Kuna miradi viporo mingi sana katika Halmashauri zetu ukiangalia Sekta ya Afya utakutana
Maboma mengi ambayo yangekamilika yangetumika kama Zahanati au Vituo vya Afya,
Elimu utashuhudia magofu ya kutosha ambayo yangekamilika yangetumika kama vyumba
vya madarasa hii yote ni kutokana na kupanga miradi mingi kwa wakati mmoja sasa kwa
mwaka huu na kupitia Kikao hiki mfanye mapitio Upya na mpange miradi michache
itakayokamilika kupitia bajeti kwa mwaka huu” Aliongeza Jafo.

Waziri Jafo alisisitiza kuwa Katika Bajeti ya LGDG mwaka huu Bil.66 zimeelekezwa kwenye
Sekta ya Afya nataka mkazisimaie mkakamilishe Maboma yaliyotelekezwa kwa kipindi kirefu
na yakamilke tayari kwa kutoa huduma halkadhalika katika maeneo mengine yote ambayo
Fedha hizi zitatumika.

Waziri Jafo alimalizia kuwa kikao hiki sio Semina wala eneo la mapumziko kwa viongozi wa
halmashauri bali ni Kikao kazi hivyo Kitumike kama fursa adhimu na muhimu ya kufanya
Mapitio ya Mipango ya halmashauri ambayo ikitekelezwa italeta matokeo Chanya na
kuwapunguzia adha wananchi wetu.

Akimkaribisha Mgeni Rasmi Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhandishi Musa Iyombe
amesema Kikao hiki ni Maalumu kwa Viongozi wote ambao wanahusika moja kwa moja na
kuwaletea wananchi maendeleo ili kwa pamoja tukubaliane, tushauriane na tuelekezane
namna bora ya kutekeleza miradi hiyo ambayo inaonekana eneo la Mipango halijafanyiwa
kazi kikamilifu.

“Viongozi wenzangu lazima suala la mipango liangaliwe kwa Makini katika Halmashauri
zetu, Jambo hili lisipofanyika kwa Umakini lina madhara makubwa kwa Jamii, litaturudisha
nyuma kimaendeleo na kila siku tutaona hatufanikiwa katika miradi yetu kwa sababu tu
tulikosa umakini katika kuandaa Mipango yetu, hebu tupitie upya mipango yetu na
tuhakikishe tunamaliza mradi mmoja kwanza kabla ya kuanza mwingine” alisema Mhandisi
Iyombe.

Akizungumza na wajumbe wa Kikao kazi Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Menejiment ya Utumishi
wa umma na Utawala bora Dkt.Laurean Ndumbaro amewakumbusha watumishi wote
kufanya kazi kwa kuzingatia Hotuba ya Mhe.Rais Dkt. John Joseph Pombe Magufuli
alipohutubia Bunge na kusisitiza Uwajibikaji, Utumishi wa Umma unaojali misingi ya
Uadilifu, Weledi wa Kitaaluma, Maadili na Uadilifu katika Utendaji kazi wetu.

“Watumishi wanapaswa kuwajibika kwa Serikali iliyopo Madarakani kwa kutekeleza yale
yote yanayowapasa kutekeleza kwa mujibu wa miongozo kwa watumishi wenzetu
tunaofanya nao kazi na kwa wananchi tunaowatumikia, tuwape haki yao ya msingi ya
kuwahudumia na kuwalete maendeleo.” Alisema Dkt. Ndumbaro.

Kupitia Kikao hiki washiriki kutoka katika Halmashauri zote watapitia Upya miradi ya
maendeleo waliyopanga kutekeleza kupitia Fedha za “LGDG” kwa kuzingatia maelekezo
watakayopewa kabla ya kupokea Fedha hizo kwa ajili ya utekelezaji.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania