CURRENT NEWS

Monday, February 26, 2018

NAIBU WAZIRI NYONGO AWAWEKA KIKAANGONI WAMILIKI WA MGODI WA NYARUGUSU MINE.

 Wananchi wakifungua njia baada waliyoifunga awali
 Diwani wa kata ya nyarugusu akimpa maelezo naibu waziri Madini Stanslaus Nyongo
 Naibu waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akiangalia mambwawa yaliyoleta madhara kwa wananchi
Mmoja wa wamiliki wa mgodi wa nyarugusu akipokea maagizo kutoka kwa Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo.
......................................................
Naibu Waziri wa madini Stanslaus Nyongo amewataka wamiliki wa mgodi wa Nyarugusu Mine  Company kulipa  fidia haraka iwezekanavyo kiasi cha sh. milionI 202 wanazoidai wakazi  wa 123 wa kijiji cha Nyarugusu.
Hata hivyo,amesema wasipofanya hivyo serikali kupitia Wizara ya madini watawanyang’anya leseni ya uchimbaji  katika eneo hilo ambapo  wawekezaji hao wanafanya  shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu.
Agizo ilo la Naibu waziri  alimelitoa baada ya wakazi hao kufunga njia ya kuingia Mgodini,.
Awali wakiwasilisha malalamiko yao kwa Naibu Waziri , mmoja wa wananchi hao Shardiraki Mashaka amesema kuwa  kipindi cha miezi 4 wamekuwa katika hali mbaya kwa kukosa chakula baada mashamba yao kuingiliwa na maji yenye sumu na kuharibu mazao yao hali iliyosababisha kukosa chakula.
Naye, Pili Ramadhani amesema mgodi huo kwa kushirikiana serikali walikuja kufanya tathimini ya uharibifu uliotokea kwenye mashamba yao na baadae wakaambiwa wafungue akaunti benki kwa ajili malipo yao lakini cha kushangaza  mmiliki wa mgodi akawajibu kuwa katika madai wanayodai  wamefanya udanganyifu kwa kuongeza maeneo na kuingiza watu ambao hawastaili kulipwa jambo ambalo sio kweli.
“Naibu waziri tumefikia uamuzi wa kuifunga njia ya kuingilia mgodini baada ya kuambiwa tutalipwa fidia lakini mpaka sasa umefika hapa hakuna lililofanyika na uongozi wa mgodi zaidi ya kutuambia tufungue akaunti kwa ajili ya malipo’’ alisema
Kadhalika, Mwenyekiti wa Kijiji Cha Nyarugusu  amekiri kuwa wananchi wake ni tangu Novemba mwaka jana mashamba yao yalingiliwa na matope yenye sumu na serikali ikafanya jitihada kubwa awali na kufanya mazungumzo na mgodi wa TFC ili walipe fidia wakakubali.
“Serikaliimefanya tathmini kwa kila muhanga na wananchi wakaendelea kuwa wavumilia sana shida ilikuja baada ya wamiliki wa mgodi kuleta barua ya kusema hawawezi kutoa fidia kwa sasa mpaka wajilidhishe kutokana na vipengele fulani hapo ndio lililipokuja tatizo,”amesema

Kufuatia hali hiyo, Nyongo amesema “Naomba istafsiriwe kuwa mlichokifanya ni makosa kufunga au kuzuia njia hii kuingia mgodini mmefanya  sawa sawa kwa sababu mnadai haki yenu, nilikuwa namtafuta huyu mzungu toka jana lakini ninataarifa polisi wamemkamata tayari,”.

Ameagiza uongozi wa mgodi huyo kushirikiana na Mkuu wa wilaya ya Geita kumaliza tatizo hilo ndani ya wiki moja kwa kuhakikisha wanalipa madai ya wananchi hao tofauti na hivyo kama wizara watachukua  hatua za kinidhamu dhidi ya mgodi uho wa Nyarugusu.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania