CURRENT NEWS

Wednesday, February 21, 2018

NAIBU WAZIRI NYONGO ATOA VIFAA VYA MICHEZO MASWA

 Naibu Waziri wa Madini Staslaus Nyongo ambaye pia ni Mbunge wa Maswa Mashariki akikabidhi mipira.......................................................................
Naibu Waziri wa Madini Staslaus Nyongo ambaye pia ni Mbunge wa Maswa Mashariki amekabidhi mipira kwa Timu zinazoshiriki Ligi Daraja la nne katika Wilaya Hiyo ambayo inaendelea kutimua vumbi katika uwanja wa nguzo nne.

Akibidhi mipira hiyo, Mhe. Nyongo amesema kuwa anatarajia ligi  hiyo itakuwa yenye ushindani  wa hali  ya juu kwa sababu inahusisha timu za wilaya hiyo na kukiomba Chama Moura Wilaya ya Maswa kuyasimamia vizuri Mashindano hayo.

''Ninachowaomba viongozi wa Chama viongozi wa Chama Cha Mpira simamieni mashindano haya kwa haki bila fitina wala mizengwe kwasababu sisi si familia moja,''amesema
 
Kwa upande wake, Katibu wa Chama cha mpira Maswa Kirunga Joseph ameshukuru msaada waliupata kupitia Mbunge kwasababu kukosekana kwa Mipira ililazimika ligi Kusimama.


Naye, Kapteni wa Timu ya Vijana Salum Said amelitaka Shirikisho la Soka Nchini kuhakikisha wanapata vifaa ili kuinua kiwango cha mpira wilaya ya maswa wasijikite maeneo ya mijini tu. 
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania