CURRENT NEWS

Friday, February 23, 2018

UTOROSHWAJI MADINI HUKUBALIKI HATA KIDOGO- NYONGO

 Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akizungumza 
 Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akikagua
..........................................................
Naibu Waziri wa Madini Stanlaus Nyongo amekemea tabia ya baadhi watendaji waliopo katika viwanja vya ndege kukosa uzalendo katika kulinda rasilimali za Taifa.

Rai hiyo ameitoa leo akiwa katika ziara yake Geita baada ya kupatiwa taarifa kuwa kuna Mtanzania amekamatwa akiwa na kilogramu 32 za dhahabu ambazo zimesafirishwa kupitia Uwanja wa ndege wa Mwanza.

Nyongo  amesema utoroshwaji wa madini haukubaliki na kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama kudhibiti utoroshaji huo unaofanywa kupitia viwanja vya ndege.

“Tunaangalia namna bora ya kudhibiti utoroshwaji wa madini na hii itasaidia kuinua uchumi wa nchi kwa kiwango kikubwa sana kweli haya mambo yanayofanyika hayakubaliki hata kidogo,’’amesema Nyongo

Naye, Mkuu Mkoa wa Geita Robert Gabriel amemuomba Naibu Waziri wa madini kuunda kwa kamati maalum ya kuchunguza kwa kina utoroshwaji  wa Madini unafanyika Kwa Kiwango Kikubwa na anaamini hata mtu akikamatwa uwanja wa Ndege wa Nairobi atakuwa  alitoka  katika Mkoa wa Geita ambao una dhahabu kwa wingi kuliko  mikoa mingine yote.

Aidha amesema kuwepo kwa mianya hiyo ya  utoroshaji wa madini kuna sababisha kuikosesha mapato stahiki serikali.

“Hali hii inatokana na kuwapo shughuli za uchenjuaji ambazo zimekuwa zikifanyika pasipo uwepo wa sheria zinazowatambua wachimbaji wadogo na kama zingekuwepo leseni ndogo zingeweza kusaidia kukusanya mapato ya kutosha na kuongeza mapato kwenye uchumi wa nchi,”amesema


Aidha ameiomba Serikali kuiangalia ofisi ya madini Geita kwa upekee ikiwa ni pamoja na kuiboresha na kuipatia vitendea kazi vya kutosha.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania