CURRENT NEWS

Monday, February 5, 2018

UWT WAADHIMISHA MIAKA 41 KWA KUTOA MISAADA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO MRIJO.

 Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dodoma Neema Majule  akikabidhi misaada kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chemba Dk.Mashimba kwa ajili ya waathirika wa mafuriko.

 baadhi ya viongozi wakiangalia maeneo yaliyoathiriwa na Mafuriko
 Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dodoma Neema Majule akiwa katika picha mjumbe wa baraza la UWT Taifa Chiku Mugo katikati yao ni mama mwenye ulemavu wa Mrijo chini aliyeathirika na mafuriko hayo.
 Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dodoma Neema Majule akivishwa vazi la kimila mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Mrijo chini kilichopo wilaya ya Chemba mkoani Dodoma alipoenda kuwapa pole na misaada waathirika wa mafuriko.

 Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dodoma Neema Majule akizungumza na akina na waathirika wa mafuriko alipoenda kukabidhi misaada iliyotolewa na jumuiya hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 41 ya kuzaliwa CCM.
Baadhi ya wakazi wa Mrijo chini walioathirika wa mafuriko wakimsikiliza mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dodoma Neema Majule hayupo pichani.
..........................................................................................................................................
UMOJA wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoani Dodoma umeadhimisha miaka 41 ya kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kutoa misaada mbalimbali kwa waathirika wa mafuriko kwenye kijiji cha Mrijo chini wilayani Chemba.

Wananchi wa kijiji hicho wapato 4,060 waliathirika na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha mkoani Dodoma mapema mwaka huu na kusababisha maji kuzingira makazi yao ambapo jumla ya  kaya 174 zinaishi kwenye mahema.

Akizungumza wilayani humo  wakati akikabidhi misaada hiyo Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dodoma Neema Majule amesema baada ya kusikia mafuriko yametokea kwenye kijiji hicho UWT Mkoa wa Dodoma iliamua kutafuta namna ya kuwasaidia waathirika.

“Sisi UWT kwa kutambua kuwa majanga kama haya yanapotokea waathirika wakuu ni wanawake tumeona ni vyema maadhimisho ya mwaka huu tukayatumia kuwafariji wanawake wenzetu na kuwapa pole na tumewaletea baadhi ya vitu ikiwemo sukari,unga wa sembe,mahindi,sabuni na nguo,”alisema mwenyekiti huyo.

Ametoa wito kwao kukubali kuhama kwenye maeneo hatarishi kwenda kuishi kwenye maeneo watayopangiwa na serikali na waendelee na shughuli za kilimo ili kiwasaidie kupata chakula na kuahidi kuwa pamoja nao endapo nao watajishughulisha.

Kwa upande wao wabunge wa  Viti Maalum Felister Bura na Fatma Taufiq wamesema ni jambo la kushukuru Mungu kwa kuwa hakuna madhara ya binadamu yaliyotokea licha ya wananchi kuzingirwa na maji kwa siku tatu na kuhimiza wananchi hao kupatiwa maeneo mapema ili waanze kujenga makazi yao ya kudumu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba dokta Semistatus Mashimba amesema tayari wataalamu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma wameanza kupima maeneo watakayopewa wananchi hao ambayo watapewa bure na kwa sasa tayari wamepokea mbegu za mahindi na alizeti ambazo watazigawa kwa wahanga hao ili warejee kwenye kilimo.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania