CURRENT NEWS

Tuesday, February 27, 2018

WACHIMBAJI WADOGO NYAKAFURU WATAKIWA KUJILINDA NA MAGONJWA YA MLIPUKO

Baadhi ya wachimbaji wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo.

 Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akizungumza na wachimbaji wadogo wa kijiji cha Nyakafulu wilaya ya Mbongwe wakati alipokuwa kwenye ziara yake ya kikazi mkoani Geita.
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akizungumza na wachimbaji wadogo wa kijiji cha Nyakafulu wilaya ya Mbongwe wakati alipokuwa kwenye ziara yake ya kikazi mkoani Geita.
........................................................................................
NAIBU Waziri wa madini Stanslaus Nyongo amewataka wachimbaji wadogo wa mgodi wa Nyakafulu uliopo wilayani  Mbogwe mkoani Geita kudumisha amani na utulivu katika mgodi huo ikiwemo usafi wa mazingira ili kuepukana na magojwa ya mlipuko.
Hata hivyo amesema iwapo hawatazingatia hayo mgodi huo utafungwa.
Akizungumza na wachimbaji hao, Nyongo amewataka wachimbaji hao kuzingatia amani na afya zao kwani ndio utaratibu uliowekwa na serikali iwapo ikitokea kukatokea magonjwa ya mlipuko kama  kipindupindu mgodi huo utafungwa  mara moja.
Hata hivyo aliwataka wachimbaji hao kuzigatia sheria na taratibu za nchi kila mtu achimbe kwa kuzingatia taratibu na sheria kwani hakuna mwenye leseni ya eneo ili hivyo haitaji kusikia mtu akinyanyaswa wala kudhulumiwa.
“Mpo hapa  kwasababu ya kauli ya Mh. Rais wa Jamhuri  ya muungano wa Tanzania mh. John Magufuli lakini vilevile akisikia kwamba hapa hakuna  amani na sio wasafi  mimi nitatoa amri ya kufunga mgodi huu kwani wizara yangu ndio inahusika  kutoa leseni hivyo pamoja na hayo  yote amani itawale”alisema Naibu waziri.
Aidha  aliwakumbusha kulipa kodi ili waweze kuchimba kwa kufata  utaratibu, sheria, na kanuni za nchi bila bugudhi  yoyote na wangawane kwa utaratibu bila kudhulumiana kwa sababu sehemu wanayochimba kuna leseni ya mtu kwaiyo wachimbe kwa kuweka akiba ili na wao baadae wakate leseni zao za uchimbaji
‘’ wachimbaji mmekuwa na tabia ya kula bata na kuhonga pesa zote mnapouza madini acheni tabia hiyo  wekeni akiba mkate leseni zenu za uchimbaji.
Pia aliunda kamati itakayokuwa chini ya Mkuu wa wilaya itasimamia  suala la kugawana asilimia ambapo kwa upande wa wasimamizi wa mgodi huo Isanja badugu watakuwa wawili watu wawili kutoka kwa wachimbaji na watu wengine wawili kutoka kwa wenye mashamba wachanguane wapange namna ya kugawana asilimia kwa amani.
Aidha wachimbaji hao walimuomba Naibu waziri wa madini kuwasaidia kupata leseni ikiwa ni pamoja na kuboresha mazingira yao na vitendea kazi kwasababu wamekuwa wakitumia njia za asili katika kufanya shughuli zao za uchimbaji.
Machimbo hayo Nyakafu  ambayo yanakadiliwa kuwa na wachimbaji elf mbili kutoka sehemu mbalimbali ambapo swala usafi wa limekuwa ni changamoto kwa kukosekana vyoo na maji safi.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania