CURRENT NEWS

Tuesday, February 6, 2018

WANANCHI WA MKAMBA WAISHUKURU SERIKALI

   
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo akizungumza  na wananchi wa kijiji cha Mkamba wilayani mkuranga


 Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo akiwa na baadhi ya viongozi wa Mkuranga na mkoa wa Pwani akifanya ukaguzi wa bonde korofi la mkuruili linalo unganisha barabara ya mkamba kwenda Msanga.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo akikagua utoaji wa huduma za afya katika kituo cha afya Mkamba.

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo  akiwa na baadhi ya viongozi walio shiriki ukaguzi wa barabara ya mkamba kwenda Msanga ambayo inahitaji matengenezo makubwa
............................................................
Wananchi wa kata ya Mkamba wilayani Mkuranga wameishukuru serikali kuwa kuwapatia fedha za kuboresha kituo chao cha afya. 

Shukrani hizo zimetolewa na wananchi hao wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo alipotembelea kijijini hapo.

Akizungumza na wananchi wa kata ya Mkamba Waziri Jafo amewapongeza wananchi hao kwa kuanza maandalizi ya ujenzi wa miundombinu itakayojengwa na fedha hizo zilizo tolewa na serikali. 

Jafo amempongeza mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Abdullahi Ulega kwa kupeleka kilio cha wananchi wa Mkamba hadi serikali kufanya maamuzi ya kupeleka milioni 400 za ujenzi wa miundombinu na milioni 300 zingine zimepelekwa MSD kwaajili ya ununuzi wa vifaa. 

Aidha, Jafo amewaagiza viongozi wa Mkuranga kwenda kujifunza katika kituo cha afya Maneromango kilichopo wilayani Kisarawe ili waone jinsi matumizi ya force account yalivyoleta manufaa katika ujenzi wa vituo vya afya hapa  nchini.

Baada ya kikao na wananchi wa Mkamba Waziri Jafo alifanya ukaguzi wa barabara inayounganisha wilaya ya Mkuranga na wilaya ya Kisarawe kupitia bonde la Mkuruili na amewaagiza mameneja wa TARURA wa wilaya ya  Mkuranga na wilaya ya Kisarawe kukaa pamoja kuiwekea mikakati barabara hiyo ili wananchi wa maeneo hayo waweze kuunganishwa vyema.


 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania