CURRENT NEWS

Monday, March 5, 2018

BITEKO: TUFANYE SIASA ZA MAENDELEO KWA WANANCHI

 Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akihutubia wananchi wakati wa mkutano wa hadhara wa Kijimbo uliofanyika katika Kijiji cha Shibingo Kata ya Yogelo, Jana 3 Machi 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Shibingo Kata ya Yogelo Mkoani Geita wakimsikiliza kwa makini Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akiwa katika ziara ya Kijimbo kusikiliza kero za wapiga kura wake, Jana 3 Machi 2018. Pamoja na mvua kunyesha lakini baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Shibingo Kata ya Yogelo Mkoani Geita wakifatilia kwa karibu na umakini mkubwa mkutano ulioitishwa na Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko wakati akiwa katika ziara ya Kijimbo kusikiliza kero za wapiga kura wake, Jana 3 Machi 2018. Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akiwaeleza Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Shibingo Kata ya Yogelo Mkoani Geita waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara juu ya namna bora ya kuwa na mafanikio kama Taifa kwa kufanya kazi kwa bidii, Jana 3 Machi 2018. Na Mathias Canal, Geita Wanasiasa hasa wasomi na wale wenye ushawishi mkubwa nchini wametakiwa kuacha kulalamika na kutoa kauli ambazo hazitawasaidia wananchi katika kuwatatulia matatizo na kero zao bali waungane na serikali katika juhudi zinazoonekana za kuleta maendeleo. Rai hiyo imetolea na Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi uliofanyika katika Kijiji cha Shibingo Kata ya Yogelo akiwa katika ziara ya kijimbo ya siku nne. Mhe Biteko amesema baadhi ya wanasiasa maarufu wamekuwa wakitumia muda mwingi kueleza matatizo na kero za wananchi bila ya kuonyesha suluhisho au kusaidia kutatua kero hizo jambo ambalo halimsaidii mwananchi kwa namna yoyote. Alisema kuwa Maendeleo ni majumuisho ya mwendelezo wa shughuli za kujiongezea kipato, amani ya nafsi na uhuru ambapo Maendeleo yeyote ambayo hayana mwendelezo wa amani ya nafsi, kipato na uhuru, hayo si maendeleo bali ni mabadiliko yenye ukomo ambayo kwayo hayaleti amani ya nafsi na uhuru wa kudumu bali kipato cha muda mfupi na furaha ya muda mfupi na mwisho wake ni mshangao wenye haiba ya huzuni ambatano na maswali yasiyo na majibu. "Maendeleo ni mchakato mi sidhani kama kuna watu hapa ambao wamekamilisha kila jambo katika familia zao, ila kila siku mnapanga na mnatekeleza jambo moja baada ya jingine, sasa watakuja watu hapa watasema watawaletea kila kitu kijijini kwenu, sasa kwa mtazamo wenu jambo hilo linawezekana kweli? wananchi wakaitikia HAPANA" Mhe Biteko alisisitiza kuwa katika kukuza uchumi wa Taifa na mtu mmoja mmoja wananchi wanapaswa kutambua kuwa wana jukumu kubwa la kushadihisha maendeleo hayo kwa kufanya kazi kwa weledi. Aidha, Mhe Biteko aliwaeleza wananchi kuwa wanapaswa kufanya mambo mawili kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano na wasaidizi wake wote, Mosi ikiwa ni kuunga mkono juhudi za utendaji lakini pili ni kumuombea ili atomize matakwa ya wananchi na kusudio la ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020. MWISHO. CODES...!
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akihutubia wananchi wakati wa mkutano wa hadhara wa Kijimbo uliofanyika katika Kijiji cha Shibingo Kata ya Yogelo, Jana 3 Machi 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Shibingo Kata ya Yogelo Mkoani Geita wakimsikiliza kwa makini Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akiwa katika ziara ya Kijimbo kusikiliza kero za wapiga kura wake, Jana 3 Machi 2018.
Pamoja na mvua kunyesha lakini baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Shibingo Kata ya Yogelo Mkoani Geita wakifatilia kwa karibu na umakini mkubwa mkutano ulioitishwa na Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko wakati akiwa katika ziara ya Kijimbo kusikiliza kero za wapiga kura wake, Jana 3 Machi 2018.

Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akiwaeleza Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Shibingo Kata ya Yogelo Mkoani Geita waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara juu ya namna bora ya kuwa na mafanikio kama Taifa kwa kufanya kazi kwa bidii, Jana 3 Machi 2018.

Na Mathias Canal, Geita

Wanasiasa hasa wasomi na wale wenye ushawishi mkubwa nchini wametakiwa kuacha kulalamika na kutoa kauli ambazo hazitawasaidia wananchi katika kuwatatulia matatizo na kero zao bali waungane na serikali katika juhudi zinazoonekana za kuleta maendeleo. 
Rai hiyo imetolea na Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi uliofanyika katika Kijiji cha Shibingo Kata ya Yogelo akiwa katika ziara ya kijimbo ya siku nne.
Mhe Biteko amesema baadhi ya wanasiasa maarufu wamekuwa wakitumia muda mwingi kueleza matatizo na kero za wananchi bila ya kuonyesha suluhisho au kusaidia kutatua kero hizo jambo ambalo halimsaidii mwananchi kwa namna yoyote.
Alisema kuwa Maendeleo ni majumuisho ya mwendelezo wa shughuli za kujiongezea kipato, amani ya nafsi na uhuru ambapo Maendeleo yeyote ambayo hayana mwendelezo wa amani ya nafsi, kipato na uhuru, hayo si maendeleo bali ni mabadiliko yenye ukomo ambayo kwayo hayaleti amani ya nafsi na uhuru wa kudumu bali kipato cha muda mfupi na furaha ya muda mfupi na mwisho wake ni mshangao wenye haiba ya huzuni ambatano na maswali yasiyo na majibu.
"Maendeleo ni mchakato mi sidhani kama kuna watu hapa ambao wamekamilisha kila jambo katika familia zao, ila kila siku mnapanga na mnatekeleza jambo moja baada ya jingine, sasa watakuja watu hapa watasema watawaletea kila kitu kijijini kwenu, sasa kwa mtazamo wenu jambo hilo linawezekana kweli? wananchi wakaitikia HAPANA"

Mhe Biteko alisisitiza kuwa katika kukuza uchumi wa Taifa na mtu mmoja mmoja wananchi wanapaswa kutambua kuwa wana jukumu kubwa la kushadihisha maendeleo hayo kwa kufanya kazi kwa weledi.

Aidha, Mhe Biteko aliwaeleza wananchi kuwa wanapaswa kufanya mambo mawili kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano na wasaidizi wake wote, Mosi ikiwa ni kuunga mkono juhudi za utendaji lakini pili ni kumuombea ili atomize matakwa ya wananchi na kusudio la ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020.

MWISHO.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania