CURRENT NEWS

Tuesday, March 27, 2018

HABARI PICHA:KAMATI YA BUNGE YA UTAWALA YAENDELEA NA VIKAO VYAKE MJINI DODOMA.

Baadhi ya Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakifuatilia mazungumzo wakati wa kupokea na kujadili Taarifa kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2017/2018 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019. Kutoka kushoto ni Mhe. Lucia Mlowe, Mhe. Saada Mkuya, Mhe. Mwantum Haji na Mhe. George Lubeleje

 Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Saada Mkuya akizungumza na Wajumbe wa kamati hiyo pamoja na viongozi wakuu kutoka Mkoa wa Simiyu (hawapo kwenye picha) walioongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka wakati wa kupokea na kujadili Taarifa kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2017/2018 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 katika kikao kilichofanyika leo ukumbi wa Pius Msekwa Mjini Dodoma. Kushoto ni Mjumbe wa kamati, Mhe. Lucia Mlowe.
 Makamu Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Mwanne Mchemba akizungumza na Wajumbe wa kamati hiyo pamoja na viongozi wakuu kutoka Mkoa wa Simiyu (hawapo kwenye picha) walioongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka wakati wa kupokea na kujadili Taarifa kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2017/2018 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019. Kulia ni katibu kamati wa kamati hiyo, Ndg. Victor Leonard

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakati wa kupokea na kujadili Taarifa kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2017/2018 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019. Kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa huo, Mhe. Jumanne Sagini


 (PICHA NA OFISI YA BUNGE)
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania