CURRENT NEWS

Saturday, March 24, 2018

JAFO ATAKA VIPAJI VYA MICHEZO VIIBULIWE NGAZI ZA CHINIWaziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akizungumza katika uzinduzi wa mashindano ya UMISETA mkoa wa Dodoma.

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akijiandaa kupiga mpira kuashiria uzinduzi wa mashindano ya UMISETA mkoa wa Dodoma.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akiwa kwenye picha ya pamoja na timu ya shule ya sekondari Makole katika uzinduzi wa mashindano ya UMISETA mkoa wa Dodoma.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akiwa kwenye picha ya pamoja na timu ya shule ya sekondari  Dodoma katika uzinduzi wa mashindano ya UMISETA mkoa wa Dodoma.

...................................................................................................................

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akisalimiana na wachezaji wa timu ya shule ya sekondari Makole katika uzinduzi wa mashindano ya UMISETA mkoa wa Dodoma.
........................................................................................
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amesema kuendelea kufanya vibaya kwa Timu za Taifa katika michezo mbalimbali kunatokana na kukosekana kwa uwekezaji wa kutosha kwenye kuibua vipaji vya michezo husika.

Akikabidhi vifaa kwa timu zitakazoshiriki mashindano ya UMISETA mjini Dodoma, Jafo amesema kuwa hali hiyo inatakiwa kufanyiwa kazi na kwamba kama ukifanyika uwekezaji mdogo kwenye michezo utaweza kuinua nchi kwenye sekta hiyo.

Waziri Jafo amesema uwekezaji kwenye michezo ni muhimu na lazima uanze kwa watoto wa shule za msingi na sekondari.

"Michezo hii haikurupuki imewekwa kwenye mpango wa Taifa upo kwenye ilani ya uchaguzi na sera za michezo ili kuhakikisha michezo inasonga mbele,"amesema.

Ameagiza kubainishwa walimu wa michezo shuleni ili kuweza kukuza kikamilifu vipaji vya michezo.

Naye,  Meneja wa Kampuni ya Coca cola wanaodhamini mashindano hayo Siha Shayo amesema watagawa vifaa vya michezo kwa zaidi ya shule 4000 zitakazoshiriki mashindano hayo mwaka huu.

Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa wilaya ya Dodoma Deogratius Ndejembi amesema uwekezaji katika michezo ngazi za chini ni muhimu.


 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania