CURRENT NEWS

Tuesday, March 27, 2018

KAIMU DC MANYONI AKABIDHIWA KOMBE LA UBINGWA WA MKOA WA SINGIDA 2018 NA TIMU YA STAND DORTMUND YA MANYONI

 Kaimu mkuu wa wilaya ya Manyoni mh Miraji Mtaturu akiwa kashika kombe la ubingwa wa mkoa wa Singida 2018 baada ya kulipokea kutoka kwa baadhi ya wachezaji wa Stand Dortmund ofisini kwake.
 Kaimu mkuu wa wilaya ya Manyoni mh Miraji Mtaturu akikabidhiwa kombe la ubingwa wa mkoa wa Singida 2018 na  baadhi ya wachezaji wa Stand Dortmund ofisini kwake.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Itigi wilayani Manyoni Ally Minja akichangia hoja kwenye mapokezi ya Kombe la ubingwa wa mkoa 2018 yaliyofanyika ofisini kwa mkuu wa wilaya.
 Mweka hazina wa wafanyabiashara wilayani  Manyoni Sultan Nasoro akichangia hoja wakati wa mapokezi ya kombe la ubingwa wa mkoa 2018 yaliyofanyika  ofisini kwa mkuu wa wilaya.
 Kaimu mkuu wa wilaya ya Manyoni mh Miraji Mtaturu akiongea ofisini kwake baada ya kupokea  kombe la ubingwa wa mkoa wa Singida 2018.
 Kaimu mkuu wa wilaya ya Manyoni Miraji Mtaturu akiwa katika picha  ya pamoja na  wadau wa michezo na baadhi ya wachezaji wa timu ya Stand Dortmund wakati wa mapokezi ya timu hiyo baada ya kutwaa kombe la ubingwa wa mkoa 2018.
Kaimu mkuu wa wilaya ya Manyoni mh Miraji Mtaturu akikabidhiwa kombe la ubingwa wa mkoa wa Singida 2018 na  baadhi ya wachezaji wa Stand Dortmund ofisini kwake.

....................................................................................................................
Kaimu mkuu wa wilaya ya Manyoni mkoani Singida mh Miraji Mtaturu amepokea kombe la ubingwa wa mkoa wa Singida kwa mwaka 2018 lililochukuliwa na timu ya Stand Dortmund ya Manyoni huku akitoa pongezi kwa wachezaji hao kwa  ushindi uliyoipata ambao umeleta heshima kubwa ndani na nje ya  wilaya hiyo.

Akipokea kombe hilo leo ofisini kwake wilayani humo mh Mtaturu amesema kama wilaya wana kila sababu ya kuwapongeza kwa ushindi huo unaotoa chachu kwa timu nyingine kuweza kufanya vizuri.

"Niwapongeze sana wachezaji,Viongozi wa timu na wadau wote kwa heshima kubwa mliotupatia, ushindi huu sio wenu peke yenu bali ni ushindi wa wilaya nzima, ahsanteni  na hongereni sana,"alipongeza mh Mtaturu.

Katika kuuunga mkono zaidi juhudi hizo mh Mtaturu ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoani humo  amechangia shilingi milioni 1  na kuahidi kuwatafutia kocha mzuri zaidi ili  awaandae wachezaji kwa ajili ya mashindano yanayokuja.

Katibu wa timu hiyo  Mohamed Bodalin akitoa neno la shukrani amesema  ushindi walioupata ni matokeo ya ushirikiano mzuri walioupata.

"Tunakushukuru sana mkuu wetu wa wilaya na ofisi yako kwa kutupokea na kwa misaada mbalimbali uliyoitoa kupitia ofisi yako ambayo kwa namna moja ama nyingine imepelekea kutwaa ubingwa huu,kwa sasa tunaenda hatua ya kanda ili kusaka nafasi ya kucheza ligi daraja la pili, tumeandaa bajeti ya sh milioni 20 tunaomba utuunge mkono,"aliomba katibu huyo.

Kwa upande wake katibu wa Chama Cha Mpira wilaya Joshua Msemakweli amewashukuru Wadau wote walioisadia timu hiyo hadi kufikia hatua ya kutwaa ubingwa wakiwemo  Ofisi ya mkuu wa wilaya, halmashauri ya Itigi, makampuni ya mabasi Super mamuu ya Manyoni, CCM Wilaya,Baba paroko  Padre Wambura wa parokia ya Manyoni,waandishi wa habari  na wadau wote.

Michango mingine iliyopatikana ni sh milioni 1.6,mchele kilo 100, vifaa vya michezo jezi set 3 na viatu vya kuchezea mpira jozi 5.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania