CURRENT NEWS

Friday, March 9, 2018

MAKILLAGI , MANYANYA WAWAFUNDA WANAWAKE WA DAR ES SALAAM UMUHIMU WA UJASILIMALI KATIKA UCHUMI WA VIWANDA

 Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Taifa(UWT), Amina Makilagi akizungumza wakati wa Warsha ya Wanawake Wajasiliamali iliyoandaliwa na Uhuru Fm katika mahadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani


 Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara  na Uwekezaji Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na Wanawake wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa Warsha ya Ujasiliamali iliyoandaliwa na kituo cha Radio cha Uhuru Fm.

 Kaimu Mkurugenzi wa Kituo Cha Radio cha Uhuru Fm, Angel Akilimali akizungumza kuwakaribisha  wanawake wajasiliamali kwenye warsha maalum iliyandaliwa kwa ajili yao


 Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara  na Uwekezaji Mhandisi Stella Manyanya akikabidhi Cherehani kwa Kaimu Mkurugenzi wa Kituo Cha Radio cha Uhuru Fm, Angel Akilimali kwa ajili ya Wanawake wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa Warsha ya Ujasiliamali iliyoandaliwa na kituo cha Radio cha Uhuru Fm.


 Mtangazaji wa kipindi Wanawake na ujasilimali cha Uhuru Fm akizungumza na Wanawake waliofika katika Warsha hiyo kujifunza mbinu mbalimbali.

 Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara  na Uwekezaji Mhandisi Stella Manyanya  na Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Taifa(UWT), Amina Makilagi  wakikagua bidhaa za Wajasiliamali waliofika katika Warsha iliyoandaliwa na Uhuru Fm.


 Wanawake wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa Warsha ya Ujasiliamali iliyoandaliwa na kituo cha Radio cha Uhuru Fm.

Mtoa mada Bi Antu Mandoza akizunguma katika Warsha iliyoandaliwa na Uhuru Fm,katika siku ya Wanawake Duniani.
 Mwakilishi kutoka VETA Tanzania Bw.Sita Peter akizungumza katika warsha kwa ajili ya kutoa mafunzo katika ya siku ya Wanawake Duniani iliyoandaliwa na Uhuru FM.
Mtoa mada kutoka Breakthrough Perfomance akizungumza na Wanawake wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa Warsha ya Ujasiliamali iliyoandaliwa na kituo cha Radio cha Uhuru Fm.


Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake ya Chama cha Mapinduzi (UWT) Amina Makillagi amewataka wanawake kudhubutu katika kuanzisha biashara hata kama kuna watu wanawakatisha tamaa.

Makillagi amesema hayo katika maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani ,ambapo Uhuru FM iliandaa mafunzo maalum kwa akina mama.

Amesema asilimia kubwa ya akina mama wamekuwa waoga kuanzisha biashara huku wengine wakisubiri kupata mitaji mikubwa kitu ambacho kimekuwa kikichelewesha maendeleo ya akina mama wengi.

Makillagi amesema kina Mama wengi uwezo wanao ,hivyo wanahitaji kuongezewe uwezo katika shughuli wanazofanya ,huku akisema kazi yake kubwa kama mbunge na katibu Mkuu wa uwt ni kiwasadia wanawake.

Akifunga mafunzo hayo Naibu Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Injinia Stella Manyanya, ameiagiza Sido kuandaa mafunzo maalum kwa akina mama hao ambao wengi wao ni wajasiriamali ili kuwasaidia katika kutengeneza bidhaa ambazo zitakubalika sokoni.

Injinia Manyanya amewataka akina mama hao kuacha uvivu kwa kuwa fursa zilizopo ni nyingi .

Katika hatua nyingine Injinia MANYANYA amewataka akina mama hao kuvunja ukimya kwa watoto wao wa kike kuhusu hedhi salama mara baada ya watoto kubalehe badala ya kuwaacha ambapo wamekuwa hawana taarifa sahihi kuhusu madadiliko hayo.

Naibu Waziri Injinia Manyanya katika sherehe hizo alikabidhi cherehani moja yenye thamani ya zaidi ya shilingi laki nne na kiasi cha shilingi laki tano.

Awali kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali amesema mafunzo hayo kwa wanawake ni endelevu ili kuwasaidia akina mama katika kuboresha shughuli zao.

 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania