CURRENT NEWS

Monday, March 5, 2018

MBUNGE WA KWANZA WA CHALINZE AVUTIWA NA MAENDELEO ANAYAYAFANYA MBUNGE WA SASA.Na shushu  Joel
Rais  mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ameahidi kutoa mifuko 300 ya sarufi katika jimbo la Chalinze  kwa ajili ya uendelezaji wa shughuli za ujenzi wa shule, Kituo cha Afya na nyumba za walimu  huko Kibindu na Kijiji cha Kwakonje katika kata ya Kibindu.

Haya aliyasema jana alipokuwa akiongea na Wananchi wa maeneo hayo na mbunge wa jimbo  hilo Ridhiwani Kikwete alipofika eneo hilo kujionea maendeleo yanayofanywa 
na wananchi wa eneo hilo kwa kushiorikiana na Mbunge wao.

Mh. Kikwete ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa jimbo hilo alisema kuwa lengo la kutoa mifuko hiyo  ni kutokana na kuridhishwa na mwenendo  mzima wa jimbo hilo kwa sasa na kujionea tofauti wake na wa sasa katika upatikanaji wa huduma za wananchi wa chalinze.

Aidha  Dkt Kikwete amempongeza mbunge huyo kwa jitihada anazofanya katika kuhakikisha wananchi wake wanapata maendeleo yenye tija na manufaa  kwa ajili ya kukuza uchumi wao.
"Wakati nikiwa mbunge kulikuwa hakuna mambo mazuri kama yalivyo sasa hivyo  wana chalinze wenzangu nawaombeni tumshike  mkono  mbunge wetu  ili atufikishe salama  kule tuendako alisema.
Naye mbunge wa chalinze amempongeza Rais Mstaafu kwa msaada huo na pia kutambua mchango  mkubwa alioufanya katika jimbo  hilo.

Aliongeza  kuwa uongozi mzuri ni ule wa kuacha  alama  katika Taifa na hili ndilo naliona mnafanya. 
Kwa Upande wa Mama Salma naye pamoja na kuchangia mifuko ya simenti naye pia aliwapongeza hasa wakina mama wa Kibindu kwa jinsi wanavyojitoa kwenye shughuli za maendeleo.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania