CURRENT NEWS

Monday, March 5, 2018

UMAKINI WAHIMIZWA TAHMINI YA MRADI WA DMDP

 Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Theresia Mbando akifungua kikao cha
Tathmini ya Utekelezaji wa Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Da r es salaam kw niaba ya
Katibu Mkuu OR-TAMISEMI Mhandisi Mussa Iyombe.
Msimamizi Kiongozi wa Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam kutoka Benki ya
Dunia Ndg. Erick Dickson akitoa maelekezo kwa washiriki wa kikao cha tathmini ya
utekelezaji wa Jiji la Dar es salaam.

 Wasimamizi wa Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es salaam wakifuatilia kwa makini
uwasilishaji wa mada mbalimbali katika kikao cha Tathmini ya Utekelezaji wa Mradi wa
Dmdp.

Katika Picha ya Pamoja na Katibu Tawala Mkoa wa Dar es salaam Bi.Theresia Mbando
}katikati} akiwa na Msimamizi Kiongozi wa DMDP kutoka Benki ya Dunia Ndg. Erick
Dickson pili}kushoto}, Mkurugenzi wa Idaya ya Uendelezaji Miji OR-TAMISEMI Ndg.
Mkuki Hante}Kwanza kushoto} pamoja na Mratibu Msimamizi wa miradi inayotekelezwa
na Beni ya Dunia chini ya OR-TAMISEMI Ndg.Davis Shemangali.
.................................................................................................
Nteghenjwa Hosseah,OR-TAMISEMI.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Mussa Iyombe
amewataka washiriki wa kikao cha Tathmini ya Utekelezaji wa Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam “DMDP” kuwa makini katika kuchambua taarifa mbalimbali za mradi
zitakazowasilishwa katika kikao hicho.

Akisoma hotuba kwa niaba ya Katibu Mkuu katika kikao hicho Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Theresia Mbando amesema kuwa tathmini hii inayofanyika kwa sasa itasaidia kutambua kwa upana wake huku ikilenga vipengelea vyote vine ambavyo vimelengwa kutekelezwa katika mradi huu.

“Mradi huu Mkubwa wenye lengo la kuboresha Jiji la Dar es salaam ili lizidi kuwa bora katika Sekta ya miundombinu, usafiri mjini, usalama, makazi bora sambamba na kujenga uwezo wa Kitaasisi pamoja na mifumo stahiki na ya kutosha kutunza kumbukumbu na takwimu itakayosaidia katika Ukusanyaji wa mapato ndio ambao tunajadili hapa leo kuangalia namna wataalamu wetu walivyusimamia na nini kimefanyika kwa kiasi gani na kwa kiwango gani” alisema Bi.Mbando.

Aidha Bi. Mbando aliongeza kuwa tunategemea mawazo yenu, hoja zenu za msingi katika
kujenga na kuboresha mipango iliyopo ya Utekelezaji wa mradi huu, ninyi kupitia Kikao hiki
mtaboresha mipango iliyopo, mtatukosoa, mrarekebisha na mtatoa mwanga wa njia gani sahihia bora ya kufuata ili mradi uweze kutekelezwa kwa mafaniko makubwa na kutatua shida za wananchi.

katika Kikao hicho mwakilishi wa Benki ya Dunia ambaye pia ndiye Msimamizi Kiongozi wa
Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam kutoka Benki ya Dunia Ndg. Erick Dickson
amesema Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Dunia wameleta Mradi
utakaobadilisha muonekano wa Jiji la Dar es Salaam.

Aliongeza kuwa tunatakiwa kuangalia kwa Makini namna ambavyo mradi huu unavyotekelezwa katika kipindi hiki cha Nusu Mwaka; Yale yaliyopangwa yametekelezwa, malengo ya mradi yamefikiwa,Wananchi wamenufaikaje kupitia mradi huuna je hakuna athari zozote za kimazingira zilizotokea bila kusahau ushiriki wa wananchi upo kwa kiasi gani.

Katika awamu ya kwanza ya mradi huu ambayo inatekelezwa kwa kipindi cha 2016 -2020 Mradi utagharimu jumla ya Dola za Kimarekani Milioni 300 ambazo ni Fedha za mradi ambazo ni Fedha za Mkopo kutoka Benki ya Dunia. 

Aidha Shirika la maendeleo la Nchi za Nordic litatoa ruzuku ya dola za kimarekani milioni Tano kwa ajili ya kukabili changamoto za mabadiliko ya Tabia ya Nchi

Wakati huo huo Serikali ya Uingereza kupitia Shirika la maendeleo la DFID linachangia ruzuku ya Paundi 25 milioni kwa ajili ya kuboresha Bonde la Mto Msimbazi na Serikali ya Tanzania inachangia dola za kimarekani milioni 25 kwa ajili ya ulipaji wa fidia kwa wananchi wanaoathirika na mradi.

Kikao hiki cha Siku tatu kinahusisha wataalamu kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi, Wasimamizi wa mradi kutoka Benki ya Dunia, Wataalam kutoka Halmashauri zote za Mkoa wa Dar es salaam pamoja na washauri wa mradi kutoka kampuni mbalimbali zinazofanya kazi za mradi huu.


 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania