CURRENT NEWS

Thursday, March 22, 2018

USHIRIKI WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA 62 WA HALI YA MAENDELEO YA WANAWAKE UNAOFANYIKA NEW YORK MAREKANI


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
Chuo Kikuu cha Dodoma,
Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Maendeleo ya Jamii,
Jengo Namba 11,
S.L.P 573,
40478 DODOMA.

 
 

Simu Na.255-26-2963341/2963342/2963346
Nukushi: 255-26-2963348                                                         
Tovuti:www.mcdgc.go.tz           
           
                                                      
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU USHIRIKI WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA 62 WA HALI YA MAENDELEO YA WANAWAKE UNAOFANYIKA NEW YORK MAREKANI KUANZIA TAREHE 12- 23/03/2018
Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inataarifu umma kuwa; Tanzania sawa na Nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Mataifa inashiriki Mkutano wa 62 wa Hali ya Maendeleo ya Wanawake unaoendelea mjini New York, Marekani kuanzia 12 - 23 Machi, 2018.
Kwa mwaka 2018 Kaulimbiu ya Mkutano ni “Changamoto na Fursa Katika Kufikia Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wa Wanawake na Wasichana Wanaoishi Vijijini”.
Katika Mkutano huo wa 62 wa Hali ya Maendeleo ya Wanawake, Tanzania inawakilishwa na Maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamaii, Jinsia, Wazee na Watoto; Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto– Zanzibar; Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Wajumbe wengine ni kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Kilimo.
                                                                                                                                               Ushiriki wa Nchi ya Tanzania kwenye Mkutano wa 62 wa Hali ya Maendeleo ya Wanawake unaondelea Nchini Marekani unatoa nafasi kwa washiri kufanya yafuatayo:
(i)                       Kutoa maoni na mapendekezo kwenye kikao cha majadiliano ya Mawaziri wa Masuala ya Maendeleo na Haki za Wanawake kuhusu utekelezaji wa vipaumbele vya Kaulimbiu kuanzia tarehe 12 - 13 Machi 2018.
(ii)                     Kuwasilisha Taarifa ya Nchi kuhusu juhudi za Taifa katika kutekeleza vipaumbele vya Kaulimbiu kwenye Kikao kilichofanyika tarehe 14 Machi, 2018.
(iii)                   Kuandaa vikao kazi vilivyotoa fursa kwa washiriki kutoa maoni kuhusu agenda ya “Jitihada za Kufikia Usawa wa Kijinsia Nchini Tanzania” kilichofanyika tarehe 14 Machi, 2108 kwa lengo la kubadilishana uelewa kuhusu mifano bora iliyofikiwa.   
(iv)                   Kushiriki midaharo mbalimbali iliyoandaliwa na nchi na taasisi nyingine kwa lengo la kujenga uelewa wa pamoja na kuiga mifano bora kwa ajili ya kuleta mabadiliko Nchini Tanzania; na
(v)                     Kushiriki katika majadiliano ya utekelezaji wa masuala, maoni na mapendekezo ya uzingatiaji wa vipaumbele katika kuendeleza hali za maendeleo ya wanawake kwenye Mkutano wa 62 wa mwka 2018.

Jitihada zilizofanyika katika kuwezesha kufikiwa kwa Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wa Wanawake na Wasichana Nchini Tanzania
Akitoa ufafanuzi kwa vyombo vya habari katika Mkutano huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga amebainisha kuwa  hatua mbalimbali zimechukuliwa katika kufikia usawa  wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake na wasichana kiuchumi wanaoishi maeneo ya vijijini. Juhudi zilizofanyika ni kama ifuatavyo:
(i)                       Tanzania imefanya uwekezaji mkubwa katika ujenzi wa miundombinu ya reli na barabara na vyanzo vya nguvu za nishati miradi ambayo itawezesha upatikanaji wa huduma bora za usafiri kwa wananchi wakiwemo wanawake na wasichana walioko katika maeneo ya pembezoni;
(ii)                     Tanzania inatekeleza Mpango Mkakati wa Kitaifa wa Miaka Mitano wa Kutokomeza Vitendo vya Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto kwa lengo la kupunguza madhara ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2022.
(iii)                   Tanzania imeaandaa na kuridhia sera na sheria ambazo zinatoa nafasi zaidi kwa wanawake na wasichana wanoishi vijijini kuweza kupata fursa ya kunufaika na huduma za kijamii, kisiasa na kiuchumi na hivyo kuongeza haki na usawa wa kijinsia. Kwa kipindi cha mwaka 2017, Sera ya Mikopo na Taasisi za Fedha na Sheria ya Msaada wa Kisheria zimeandaliwa na kufanyiwa marekebisho ili kuweka mazingira wezeshi kwa wanawake.
(iv)                   Tanzania imechukua hatua mbalimbali za kuwawezesha wanawake kiuchumi ikiwa ni pamoja na utoaji wa mikopo yenye riba nafuu, utoaji wa mbinu za ujasiriamali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake, na kuanzisha shughuli mbalimbali zinazochochea ongezeko la kipato kwa wanawake. Hatua hizi na nyingine nyingi zimewezesha Tanzania kutajwa na ‘Taasisi ya Kimatifa ya Uchumi’ kuwa ni kinara wa ukuaji wa uchumi jumuishi ikiongoza kati ya Nchi zote za Afrika kwa mwaka 2018.
(v)                     Utoaji wa elimu bure kuanzia Shule ya Msingi hadi kidato cha Nne kumechangia uwiano sawa wa kijinsia katika uandikishaji wa wavulana na wasichana wanaojiunga na za Shule za Msingi na Sekondari;
(vi)                   Tanzania imarisha huduma za afya ikiwemo uboreshaji wa afya ya mama na mtoto katika vituo vya afya pamoja na kuanzisha maduka ya Serikali ya Dawa kwa kuongezewa bajeti kwa kiasi cha asilimia 935.
Imetolewa na:

KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO


 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania