CURRENT NEWS

Tuesday, March 27, 2018

WANANCHI WASHAURIWA KUTUMIA VIZURI FEDHA ZA TASAF

  Wanufaika wa Tasaf

................................................................................................................
Na Shani Amanzi,

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Dkt. Semistatus Mashimba amewataka Wananchi wa Wilaya ya Chemba kuweka kipaumbele suala la Afya hasa kwenye kujiunga na kadi ya
bima ya Afya ambayo ya kiwango cha chini(CHF).

Mashimba amesema “Itakuwa jambo jema kama
leo hii pesa hizi za TASAF mnazopewa mtazitumia pia katika kujiunga na bima ya Afya
kwani Serikali ya Awamu ya Tano ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wamezidi
kuboresha huduma za Afya ikiwemo kupunguza kiwango cha upatikanaji wa bima ya
Afya ambacho kiwango cha chini ni elfu 13000/=”

Dkt.Mashimba aliyazungumza hayo alipokuwa anafanya ziara na Viongozi wa Serikali na
wa Siasa katika zoezi la kugawa pesa za TASAF katika kaya maskini katika vijiji
mbalimbali ikiwemo kijiji cha Igunga tarehe 21/3/2018 na kuzungumza na Wananchi wa
kijiji hicho.

Naye Mratibu wa Tasaf wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Ndg.Simon Butondo
amesema TASAF awamu ya Tatu inatekeleza programu inayoitwa “Mpango wa
Kunusuru Kaya Maskini ni mpango wa kitaifa wa kunusuru kaya Maskini unaolenga
kuongeza kipato na kutoa fursa kwa kaya maskini kwa kupewa ruzuku ya fedha ili
kupunguza kiwango cha umaskini.

Aidha Mpango huo unalenga kutoa miundombinu ya Afya,Elimu na Maji ili kuboresha
lishe,kuwezesha kununua mahitaji ya Wanafunzi na uzinduzi rasmi wa TASAF III ,Wilaya
ya Chemba ulifanywa 11/4/2014.

Hata hivyo zoezi hilo huwa linafanyika kila baada ya miezi miwili ambapo wanaangalia
kigezo kikubwa ni kaya maskini na idadi ya watoto waliopo katika familia.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania