CURRENT NEWS

Tuesday, April 24, 2018

DC MTATURU AMSHUKURU RAIS MAGUFULI KWA KUTOA FEDHA ZA UJENZI WA OFISI YA DC.


 Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akijadiliana jambo na Dk.Medard Kalemani wakiwa  kwenye kijiji cha Nkunikhana.

 Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida Miraji Mtaturu akiomba kufikishiwa salamu za shukrani kwa Rais kutokana na fedha za ujenzi wa ofisi ya mkuu wa wilaya.

Wananchi wa kijiji cha Nkhuninkana wakimsikiliza mgeni rasmi Dk.Medard Kalemani wakati akiongea na wananchi kabla ya kuzindua uwashaji wa umeme kijiji cha Nkunikhana wilayani humo.
      ...........................................................
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida Miraji Mtaturu amemshukuru Rais Dk.John Pombe Magufuli kwa kuwapelekea shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya mkuu wa wilaya.

Mbali na fedha hizo pia amepeleka shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya kuanzisha ujenzi wa hospitali ya wilaya zilizotengwa kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018.

Mtaturu amesema hayo hivi karibuni wakati wa ziara ya waziri wa Nishati Medard Kalemani alipoenda kukagua miradi ya umeme wilayani humo.

"Mh waziri pamoja na kwamba mh rais ametuweka kwenye mpango wa miradi ya REA mwaka huu lakini pia ametuletea pesa kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Dc na hela za kuanzisha ujenzi wa hospitali ya wilaya,
Hii ni hatua kubwa na ya kupongezwa,tunakuomba sisi wakazi wa Ikungi utufikishie shukrani  zetu  nyingi sana na tunamuahidi kuendelea kumuunga mkono katika juhudi zake za kuwaletea wananchi maendeleo,"alisema Mtaturu.

Amewaomba wakazi wa Ikungi kumlipa fadhila mh Rais kwa kufanya kazi kwa bidii kama kauli mbiu yake inavyosema ya Hapa Kazi tu.

Ujenzi wa hospitali ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inayosisitiza kuwa na hospitali kila wilaya.

Wilaya ya  Ikungi ilianzishwa tarehe 08 March, 2013 katika tangazo la gazeti la serikali no 87.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania