CURRENT NEWS

Saturday, April 14, 2018

DC SHEKIMWERI AHIMIZA JAMII KUSHIRIKI UJENZI WA MIRADI YA MAENDELEO. Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri akiwapa pole na kuwafariji wagonjwa waliolazwa katika kituo cha afya cha Kibakwe.


 Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma Jabir Shekimweri akiwa na kamati ya ulinzi na usalama wakishiriki kwa vitendo ujenzi wa wodi ya akina mama na watoto katika kituo cha afya cha Mima.


 Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Kibakwe alipowatembelea shuleni hapo na kuwatakia maandalizi mema ya mitihani yao.


 Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri pichani akiwatakia kheri ya mtihani wa mock na ile ya kitaifa itakayofanyika baadae mwaka huu wanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Pwaga iliyopo wilayani humo.


Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma Jabir Shekimweri akiwa na kamati ya ulinzi na usalama wakishiriki kwa vitendo ujenzi wa wodi ya akina mama na watoto katika kituo cha afya cha Mima.
....................................................................................................
Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma Jabir Shekimweri amefanya ziara ya kukagua miundombinu katika sekta ya Afya, Barabara na Elimu na kushiriki katika ujenzi wa wodi ya akina mama na watoto katika kituo cha afya cha Mima kilichopo wilayani humo.

Akishiriki ujenzi huo ameihimiza jamii kutoa ushirikiano kwa kutambua kuwa miradi hiyo ya umma ni ya kwao hivyo wanapaswa kuimiliki kwa mustakabali wa afya zao.

"Nitumie nafasi hii kuwahimiza Kamati za Ujenzi kujituma,kizingatia uzalendo,Sheria na Taratibu za Manunuzi na Matumizi ya Umma katika kutekeleza majukumu yenu", alisema mkuu huyo.

Aidha amewataka Wataalamu wa Halmashauri hususani Wahandisi wa Ujenzi kuongeza kiwango cha usimamizi ili ubora wa hali ya juu na thamani ya fedha ionekane katika miradi hiyo.

Mkuu huyo wa wilaya amewanyooshea vidole Viongozi wa Kisiasa ambao baadhi yao wanalalamikiwa kutaka kuhodhi usimamizi wa miradi kwa maslahi yao binafsi na kusisitiza kuwa kamwe hatosita kuwachukulia hatua za kisheria.

Mkuu huyo wa Wilaya ambaye aliambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama amewataka kufanyia kazi ushauri uliotolewa katika ziara hiyo ambayo ni endelevu hadi miradi hiyo itakapokamilishwa mwishoni mwa Mwezi wa Sita mwaka huu.

Kwa kutambua wingi wa wanafunzi na uhitaji wa Bweni la Wanafunzi wa Kike katika Shule ya Sekondari  iliyopo Kibakwe, amewaomba na kuongoza harambee ndogo ya kuchangia Ujenzi wa Bweni hilo ambapo kiasi cha Shilingi milioni mbili zilipatikana papo hapo.

Mh Shekimweri  ametumia ziara hiyo kuwatembelea wanafunzi wa kidato cha sita wa shule wa sekondari ya Kibakwe na kuwatakia maandalizi mema ya mitihani yao ya mwisho.

Hali kadhalika, amewatembelea wanafunzi wa shule ya sekondari ya Pwaga na kuwatakia maandalizi mema ya mitihani ya Mock na ile ya kitaifa itakayofanyika baadae mwaka huu na kuwahimiza kusoma kwa bidii kwa lengo la kufaulu la kwenda kidato cha tano.

 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania