CURRENT NEWS

Sunday, April 22, 2018

JPM KUZINDUA MIRADI YA MAENDELEO DODOMA

RAIS John Magufuli leo anatarajiwa kuwasili mkoani Dodoma kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kiserikali ikiwemo kuzindua  miradi mbalimbali ya maendeleo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk.Binilith Mahenge kwa waandishi wa habari, amesema siku ya jumatatu Rais Magufuli atazindua jengo la Mfuko wa Pensheni wa PSPF na tawi jipya la benki ya NMB lilipo mtaa wa barabara ya Chimwaga mjini Dodoma.
Amesema Aprili 24  Rais atalihutubia  Bunge la Afrika Mashariki ambalo linafanyika Tanzania Bara hapa Dodoma.
“Siku ya Alhamis Rais atakuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zitakazofanyika katika uwanja wa Jamhuri,”amesema.
Aidha amesema Siku ya Ijumaa ya Aprili 27 Rais atazindua barabara ya Dodoma hadi Babati yenye urefu wa Kilometa 231.8 na sherehe ya uzinduzi wa barabara hiyo zitafanyika kwenye wilaya ya Kondoa eneo la Bicha.
Mkuu huyo amesema baada ya shughuli hizo Rais Magufuli  Jumapili ataondoka kulekea mkoani Iringa kwa ajili ya Sherehe za Mei Mosi kitaifa mwaka huu ambazo zinafanyika kitaifa mkoani humo.
Amewataka wakazi wa Dodoma na mikoa ya jirani  kujitokeza kwa wingi  kuhudhuria kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 54 ya Muungano na uzinduzi wa miradi.

 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania