CURRENT NEWS

Tuesday, April 17, 2018

KATIBU MKUU TAMISEMI AKABIDHI VYETI VYA PONGEZI KWA TIMU YA MAANDALIZI YA BAJETI YA MWAKA 2018/19.


Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI Eng. Mussa Iyombe(Aliyekaa Katikati) katika Picha ya Pamoja na Wakurugenzi walioshiriki kuandaa mpango wa Bajeti ya OR-TAMISEMI kwa mwaka wa Fedha 2018/19 kabla ya kuwasilishwa Bungeni

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Tawala za Mikoa Beatrice Kimoleta akitoa maelezo ya namna Timu ya Uandaaji wa Mpango wa Bajeti ilivyotekeleza jukumu hilo kwa Ufanisi.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI Eng. Mussa Iyombe(Aliyekaa Katikati) katika Picha ya Pamoja na Wataalamu walioshiriki kuandaa mpango wa Bajeti ya OR-TAMISEMI kwa mwaka wa Fedha 2018/19 kabla ya kuwasilishwa Bungeni

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI Eng. Mussa Iyombe(Aliyekaa Katikati) katika Picha na Mkurugenzi wa Sera na Mipango John Cheyo (aliyekaa kulia), Kaimu Mkurugenzi wa Tawala za Mikoa Beatrice Kimoleta (aliyekaa kushoto) pamoja na Wataalam walioshiriki kuandaa mpango wa Bajeti ya OR-TAMISEMI kwa mwaka wa Fedha 2018/19 kabla ya kuwasilishwa Bungeni

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI Eng. Mussa Iyombe(Kulia) akikabidhi cheti cha Pongezi kwa Mshiriki wa Timu ya Maandalizi ya Bajeti kwa mwaka wa Fedha 2018/19.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI Eng. Mussa Iyombe(Kulia) akikabidhi cheti cha Pongezi kwa Mshiriki wa Timu ya Maandalizi ya Bajeti kwa mwaka wa Fedha 2018/19.

...............................................
 
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa amewapongeza Watumishi walioshiriki kuandaa Bajeti ya OR-TAMISEMI ambayo ilipitishwa mwanzoni mwa wiki hii na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akiwakabidhi vyeti vya Pongezi katika kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Wizara hii Eng. Iyombe amesema watumishi walioshiriki mwaka huu katika maandalizi ya bajeti wamejitoa kwa moyo na kufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu kiasi kilichopelekea Bajeti kuwa ya viwango na inayolenga mahitaji ya wananchi.
“Umakini wenu katika maandalizi ya bajeti hii mmewezesha Bajeti ya OR-TAMISEMI kupitishwa kwa kauli moja na Waheshimiwa Wabunge wote hii inaonyesha uhalisia wa yale ambayo tumepanga kuyafanya kwa mwaka wa Fedha 2018/19” alisema Katibu Mkuu Eng. Iyombe.
Aliongeza kuwa hii inaonyesha maandalizi yalikuwa mazuri na matatizo ya wananchi ndio yaliyowekwa kwenye mpango wa Bajeti kutoka kila kona ya Tanzania changamoto za maeneo hayo zimewekwa kwenye Mpango wa Utekelezaji hilo nido la msingi zaidi na ndio maana imekuwa rahisi hata kwa Waheshimiwa Wabunge kutuamini na kupitisha Bajeti ya Wizara yetu hongereni sana kwa hili.
Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi wa Idara ya Tawala za Mikoa Beatrice Kimoleta amesema kuwa Timu hii imekuwa na nidhamu ya hali ya juu kwa sababu walichagua Mwenyekiti wao ambaye aliwasimia wakati wote kwahiyo Wakurugenzi tulipata muda wa kufanya kazi za Ofisini na huku kazi ziliendelea vizuri kabisa.
Kimoleta aliongeza kuwa nimefurahishwa sana na umoja uliokuwepo katika Timu hii ya maandalizi ya Bajeti, Nidhamu ya hali ya juu pamoja na mawasilisino ninaomba vitu hivi vilivyotupa mafanikio tuviendeleze katika maeneo yetu ya kazi na katika Timu zijazo tutakazochaguliwa kufanya kazi.
Wataalam hao waliopongezwa katika kikao hiki ni wale waliofanikisha zoezi la uchambuzi wa Mipango ya Bajeti za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa mwaka wa Fedha 2018/19 kwa Sekta zote kwa kutumia mfumo wa Planrep iliyoboreshwa.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania