CURRENT NEWS

Monday, April 23, 2018

MAVUNDE ATEKELEZA KWA ASILIMIA 70 AHADI ZAKE NDANI YA MIAKA MIWILI
 Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akizungumza wakati akisoma taarifa ya  Utekelezaji wa kazi zake kwenye Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi(CCM)Wilaya ya Dodoma Mjini kwa mwaka 2015-2017.


Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akiwasilisha taarifa ya  Utekelezaji wa kazi zake kwenye Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi(CCM)Wilaya ya Dodoma Mjini kwa mwaka 2015-2017.
 Mbunge wa Viti maalum Felister Bura akizungumza  katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi(CCM)Wilaya ya Dodoma Mjini.
  Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akipokea cheti maalum cha kutambua mchango wake alioutoa wakati wa uchaguzi wa viongozi wa CCM wilaya ya Dodoma mjini katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi(CCM)Wilaya ya Dodoma Mjini.
  wajumbe wa  kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi(CCM)Wilaya ya Dodoma Mjini.
  wajumbe wa  kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi(CCM)Wilaya ya Dodoma Mjini.


 wajumbe wa  kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi(CCM)Wilaya ya Dodoma Mjini.

Mwenyekiti wa Baraza la Wazee mkoa wa Dodoma Balozi Job Lusinde akizungumza  katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi(CCM)Wilaya ya Dodoma Mjini.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma Godwin Mkanwa akionesha mara baada ya kuzindua gazeti maalum la  Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde linalojulikana kwa jina la Jimboni Kwangu ambalo linazungumzia habari mbalimbali za jimbo hilo. 

                     ......................................................................................
Mbunge wa Dodoma Mjini Anthony Mavunde amesema hadi sasa ametekeleza zaidi ya asilimia 70 ya ahadi zake alizozitoa wakati wa kampeni mwaka 2015 na kuwahakikishia wakazi wa Jimbo lake hilo kuwa atahakikisha wanapata huduma zote muhimu kama alivyoahidi.
  
Akiwasilisha taarifa ya  Utekelezaji wa kazi zake kwenye Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi(CCM)Wilaya ya Dodoma Mjini kwa mwaka 2015-2017.
  
Mavunde amesema kwa kipindi cha miaka miwili tangu wananchi wa Jimbo hilo wamchague ameweza kutekeleza ahadi mbalimbali alizozitoa.
  
Katika kikao hicho, Mavunde ameeleza mafanikio makubwa na utekelezaji wa ahadi zake katika sekta ya elimu, Afya, Maji, Miundombinu, Nishati na Uwezeshaji wananchi kiuchumi.
  
Amewahakikishia wananchi hao kuwa ataendelea kutatua kero mbalimbali zinazowakabili katika sekta ya afya ili waweze kupata huduma bora.
  
Aidha amesema kuna uboreshaji wa miundombinu ya maji unatarajiwa kufanyika katika vijiji mbalimbali vya jimbo hilo na inakadiriwa kugharimu kiasi cha Sh.Milioni 800.
  
Ameeleza kuwa maombi mengi yamepelekwa kwa wafadhili juu ya ufadhili wa miradi ya maji mijini na vijijini.
  
Hata hivyo, amesema katika uwezeshaji wananchi kiuchumi amekuwa akitoa mafunzo ya ujasiriamali na kwasasa anatarajia kutoa kwa kila kata ili kuwapatia wananchi ujuzi.
  
Akizungumzia sekta ya ardhi, Mavunde amesema katika ardhi ameendelea kushughulikia migogoro ya ardhi ya mtu mmoja mmoja au kikundi kwa kutenga siku maalum ya kusikiliza kero za wananchi kila Alhamis ya wiki.
  
Kufuatia taarifa hiyo, Viongozi mbalimbali wa CCM wa Mkoa huo walimpongeza kwa hatua hiyo na kuwataka wabunge wengine waige mfano huo.

Katika kikao hicho pia alialikwa Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye amesema Tanzania kuna wabunge wengi sana wanaotokana na CCM lakini Mavunde anatosha sana.
  
“Ulipokuwa unasema utekelezaji wa Ilani umefanya mambo makubwa sana uliyoyafanya wananchi wa Dodoma wana kila sababu ya kushukuru, haya mazuri ambayo yameelezwa na mbunge tusijifungie tukaeleze wananchi, uendelee kuwasaidia wananchi wako,”amesema Aweso.

Amewahakikishia wananchi kuwa watapata maji safi na salama na yenye kutosheleza.


 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania