CURRENT NEWS

Friday, April 6, 2018

TIMES FM NA CLOUDS FM ZAPEWA ONYO KWA UKIUKAJI WA KANUNI ZA UTANGAZAJI.
Kamati ya Maudhui ya TCRA leo imetoa hukumu kwa vituo viwili vya radio Times FM radio na Clouds FM kwa makosa ya ukiukwaji wa Kanuni za   Utangazaji za mwaka 2018.

Times FM walitangazwa mahojiano na mwanamziki Nasib Abdul "Diamond Platinum" ambapo katika mahojiano hayo mwanamuziki huyo alitamka maneno yasiyofaa kimaudhui akimshambulia Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza. 

Kufuatia hali hiyo, Times FM wamepewa Onyo na kutakiwa kumuomba radhi Mhe.Naibu Waziri Shonza na jamii kwa ukiukwaji huo wa maadili ya Utangazaji.


Kwa upande wa Clouds FM, kituo hicho kimepewa onyo kwa kutozingatia mizania ya utoaji wa habari uliohusu pande mbili ya mwanamuziki  Ibrahim Musa "Roma mkatoliki" na Naibu Waziri Mhe. Shonza.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania