CURRENT NEWS

Monday, May 14, 2018

ACHENI UJANJA UJANJA FANYENI KAZI-JAFO

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akiwa na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zaibu Talaki akimsikiliza mkandarasi anayejenga  barabara za Manispaa ya Shinyanga.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akiwa katika ukaguzi wa barabara Shinyanga.
 Muonekano wa ujenzi wa barabara za lami katika Manispaa ya Shinyanga.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akitoa maelekezo kwa mkandarasi juu ya ukamilishaji wa barabara za Manispaa ya Shinyanga.
.......................................................
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani Jafo amemtaka mkandarasi anayejenga barabara za Manispaa ya Shinyanga Jassie & Co. Ltd kuacha Ujanja Ujanja ili akamilishe kazi ya ujenzi haraka iwezekanavyo.

Waziri Jafo ametoa kauli hiyo leo alipotembelea kukagua ujenzi wa barabara hiyo.

Jafo amesema kwamba haridhishwi kabisa na utendaji wao wa kazi kwani mkandarasi amekamilisha kilometa nne pekee kati ya kilometa 13 zinazotakiwa kujengwa. 

"Acheni Ujanja Ujanja Fanyeni kazi.Mkandarasi hakikisha unakamilisha ujenzi wa barabara hii ndani ya muda kama mkataba unavyoainisha," amesema.

Aidha, Waziri Jafo amemuelekeza mkuu wa mkoa wa Shinyanga kuendelea kufuatilia utendaji wa mkandarasi huyo ili mradi huo ukamilike kama ilivyo kusudiwa.

Mradi huo unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba mwaka huu na Manispaa ya Shinyanga ni miongoni mwa miji 18 ambayo serikali inaimarisha miundombinu kwa kujenga barabara za lami pamoja na kufunga taa za barabarani.  
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania