CURRENT NEWS

Thursday, May 17, 2018

HALMASHAURI NCHINI ZATAKIWA KUACHA MIGOGORO YA ARDHI

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo  akisaini vitabu vya wageni alipofika katika Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto na Kilindi wakati akishiriki kutatua mgogoro wa  maeneo hayo uliodumu kwa miaka 20 akiwa na Waziri wa Ardhi Mhe.William Lukuvi. 
 Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto na Kilindi Mkoani Manyara wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mheshimiwa Selemeni Jafo wakati akitoa maelekezo juu ya mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka 20.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akiongea na wananchi kuhusu maelekezo ya  serikali juu ya mgogoro wa Ardhi kati ya Halmashauri ya Kilindi na Kiteto Mkoani Manyara.
.............................................
Angela Msimbira OR TAMISEMI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo amesema migogoro ikipungua katika halmashauri nchini itasaidia kupanga mipango ya maendeleo na kuongeza uchumi na kuiwezesha Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa kutimiza wajibu wake.

Ameyasema hayo wakati akiongea na wananchi  katika utatuzi wa  Mgogoro  wa mipaka uliodumu kwa muda wa miaka ishirini katika  ya Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto iliyoko Mkoani Manyara na Kilindi Mkoani Tanga na kusababisha mauaji baina ya wakulima na wafugaji.

Amesema Halmashauri zikiwa na migogoro utekelezaji wa majukumu unakuwa mgumu na kurudisha nyuma maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla hivyo hakkuna budi wananchi wakabadilika kwa kuacha migogoro na kujadili maendeleo na jinsi ya kukuza uchumi wa nchi.

“Inasikitisha kuona Halmashauri nyingi nchini zinamigogoro ambayo hurudisha nyuma maendeleo katika jamii na kuifanya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa kutoweza kutimiza malengo yake katika kuhudumia wananchi”Amesema Jafo

Mheshimiwa Jafo amesema lengo la kuja kutatua mgogoro huo uliodumu kwa miaka 20 ni kutekeleza magizo ya Serikali hivyo wananchi wanatakiwa kuwa wamoja na kuhakikisha wanatekeleza majukumu ya kujenga uchumi wa Nchi.

Amesema anaimani kubwa kuwa mwenendo na maelekezo katika suala zima la miradi ya maendeleo lazima litafanikiwa pale wananchi wanapokuwa katika hali ya umoja na mshikamano kwa kupunguza au kuiondoa kabisa migogoro katika jamii.

Amesema kuwa  baada ya kupatiwa maelekezo  ya Serikali Wananchi wa Kilindi na Kiteto  wataendelea kushikamana kwa pamoja  kwa kufuata  maelekezo ya Serikali  na kuishi  kwa Amani  na kufanikisha masuala ya maendeleo katika jamii zao.

Mhe Jafo amewataka wananchi wa Kilindi na Kiteto kuungana  na kushirikiana pamoja ili kupunguza migogoro kwa kuwa migogoro ikiisha itasaidia kupaanga mipango ya maendeleo na kuongeza uchumi na kuiwezasha Halmashauri hizo kutekeleza majuku yao kwa ufanisi.

Aidha akiongelea kuhusu malalamiko ya wananchi wa Kibaloshi na Ilerai kuhusu kuwa na Mamlaka ya Mji mdogo Mhe. Jafo amemuagiza Mkuu wa Mkoa kusimamia sula hilo na kuwataka wananchi kukaa vikao vya kisheria vya kujadili suala hilo ili liweze kutekezwa.

 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania