CURRENT NEWS

Saturday, May 12, 2018

JAFO AAGIZA UJENZI WA KITUO CHA AFYA BWANGA UKAMILIKE NDANI YA MWEZI MMOJA.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa na viongozi wa mkoa wa Geita katika ukaguzi wa miradi ya maendeleo.

Wanafunzi wa shule ya sekondari Magufuli wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo alipokuwa katika ziara ya kukagua miundombinu ya shule hiyo.

Majengo ya kituo cha afya Bwanga 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa na viongozi wa mkoa wa Geita kwenye ukaguzi wa ukarabati wa kituo cha Afya Bwanga.
............................................................
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani Jafo ametoa mwezi mmoja kwa Mhandisi wa Ujenzi wa   Halmashauri ya Chato mkoani Geita kusimamia ipasavyo na kukamilisha Ujenzi wa miundombinu ya kituo cha afya Bwanga ambacho kimepokea Sh.Milioni 500 kutoka serikali kuu. 


Waziri Jafo ametoa agizo hilo alipokuwa wilayani Chato mkoani Geita katika ziara ya kukagua wa miradi ya maendeleo.  


Jafo amesema hajaridhishwa na kasi ya ujenzi wa kituo hicho na ametoa siku 30 kazi zote ziwe zimekamilika.


Katika hatua nyingine, Waziri Jafo amefurahishwa na ujenzi wa miundombinu katika shule ya sekondari ya kidato cha tano na sita ya Magufuli.


Shule hiyo imeimarishwa miundombinu yake ya vyumba vya madarasa, vyoo, bwalo la chakula, pamoja na mabweni. 


Akizungumza shuleni hapo, Jafo amewapongeza walimu na wanafunzi wa shule hiyo ya Magufuli kwa kuwa miongoni mwa shule 25 bora nchini  kwenye matokeo ya kidato cha sita mwaka 2017.


Waziri Jafo amewataka wanafunzi wa kidato cha sita mwaka huu kuweka jitihada zao kwenye masomo  ili shule hiyo iendelee kufanya vizuri.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania