CURRENT NEWS

Sunday, May 13, 2018

JAFO AFURAHISHWA NA MRADI WA MACHINJIO JIJI LA MWANZA

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa na Viongozi wa mkoa wa Mwanza wakikagua Miradi ya maendeleo.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akipongeza ujenzi mzuri wa barabara za changarawe katika mitaa ya jiji la Mwanza.
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Ngaza.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Ngaza.

Viongozi wa Mkoa wa Mwanza wakiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo katika ukaguzi wa miradi mbalimbali ya jiji hilo.
Machinjio inayoboreshwa katika jiji la Mwanza.

..............................................................
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amewapongeza viongozi wa mkoa na jiji la Mwanza kwa kuboresha machinjio ya Kisasa ndani ya jiji hilo. 

Jafo ametoa pongezi hizo leo alipotembelea mradi huo mkubwa ambao kukamilika kwake kutawezesha kuchinjwa ng'ombe 700 kwa siku.

Aidha mradi huo  utaongeza mapato ya jiji hilo ambapo yanatarajiwa kuongezeka kutoka Sh. milioni 30 kwa mwezi hadi Sh.milioni 120  kwa mwezi kwa chanzo hicho pekee. 

Akizungumza katika mradi huo, Waziri Jafo amezitaka Halmashauri zingine nchini kuiga utekelezaji wa mradi huo.

Aidha Waziri huyo Jafo amempongeza Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. Mongela, Mbunge wa Nyamagana  Stanslaus Mabula, Mkuu wa wilaya, pamoja na Mkurugenzi wa jiji na baraza la madiwani kwa usimamizi wa miradi na utendaji kazi wao uliotukuka.

Mbali na kutembelea mradi wa machinjio , katika ziara hiyo pia  Jafo amefanikiwa kutembelea maeneo mbalimbali ya miradi ya maendeleo ikiwemo  ukarabati wa shule ya wasichana ya Ngaza, eneo linalo tarajiwa kujengwa maegesho ya magari ya mizigo, stendi ya Nyegezi inayotarajiwa  kuboresha, miundombinu ya barabara za mawe na  Hospitali ya Nyamagana.

 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania