CURRENT NEWS

Monday, May 7, 2018

JAFO AITAKA MANISPAA YA UBUNGO WAJITATHMINI

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akizungumza na wafanyabiashara alipotembelea Soko la Shekilango kuangalia ujenzi uliofanyika.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akikagua utoaji huduma katika kituo cha Afya cha Palestina Manispaa ya Ubungo.
Wafanyabiashara wa soko la Shekilango wakiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo katika ukaguzi wa soko hilo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akikagua mfumo wa maji taka uliokarabatiwa katika Kituo cha Afya Palestina Manispaa ya Ubungo.

.........................................................
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo ameitaka manispaa ya Ubungo ijitathimini katika usimamizi wa mapato na utekelezaji wa miradi ya maendeleo. 

Jafo amesema hayo alipokuwa katika ziara ya kukagua shughuli mbalimbali za miradi ya maendeleo jijini Dar es salaam.

Akizungumza katika ziara hiyo, Waziri Jafo ameonesha kusikitishwa na manispaa hiyo kuonyesha dalili za wazi kushidwa kufunga mifumo ya kielectroniki katika maeneo yote  ya  kituo cha afya cha Palestina chenye watu wengi wanao hudumiwa. 

Amesema katika eneo la mapokezi pekee ndilo walilofunga mfumo wa kielekroniki kitendo ambacho kinakosesha mapato  makubwa kwa serikali ambapo kwasasa amejulishwa kwamba zinakusanywa sh.milioni mbili kwa mwezi. 

"Hali hii iliyojitokeza katika kituo cha Palestina kutotumika kikamilifu mifumo ya kielektroniki kunaashiria hata katika vyanzo vingine kuna uwezekano mkubwa wa upotevu wa mapato ya Manispaa ya Ubungo," amesema Jafo

Kufuatia hali hiyo, Waziri Jafo ameagiza mfumo wa GotHomis ufungwe katika maeneo yote ifikapo Mei 30 mwaka 2018. 

Aidha, Waziri Jafo amemtaka mkurugenzi wa Manispaa hiyo John Kayombo kusimamia vyema utekelezaji wa miradi katika manispaa hiyo.

Hata hivyo amesema anakusudia kuunda timu ya uchunguzi na ufuatiliaji kutoka TAMISEMI ili kujiridhisha mwenendo wa ukusanyaji wa mapato pamoja na utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa fedha ambazo Halmashauri hiyo imepokea hadi sasa.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania