CURRENT NEWS

Monday, May 14, 2018

JAFO AKEMEA WIZI WA VYUMA VYA MADARAJA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa na viongozi wa mkoa wa Tabora na wilaya ya Nzega wakikagua eneo ambalo miundombinu ya barabara itapitishwa.
 Viongozi wakikagua eneo litakapojengwa daraja la Nhombola 
Wananchi wakiwa upande wa pili wa mto katika eneo ambalo litajengwa daraja la Nhombola.
......................................................
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amekemea wananchi wenye tabia mbaya ya kuiba vyuma vinavyo wekwa katika kingo za madaraja kwamba watakapobainika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

 Jafo ametoa onyo hilo alipokuwa wilayani Nzega mkoani Tabora alipokwenda kukagua aneo la Nhombola panapotarajiwa kujengwa daraja kubwa katika mwaka wa fedha 2018/2019.

Daraja la Nhombola ni moja ya ahadi ya Rais John Magufuli ambapo katika mwaka wa fedha 2018/2019, Ofisi ya Rais TAMISEMI imetenga Sh.milioni 500 kupitia wakala wa barabara vijijini na mijini (TARURA) kwaajili ya ujenzi wa daraja hilo.

Akikagua eneo hilo, Waziri Jafo amesema baadhi ya watu wana tabia ya wizi wa vyuma ambavyo wanakwenda kuviuza kama vyuma chakavu. 

Jafo amesisitiza kwamba Serikali inatumia fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu hivyo wananchi wanapaswa kuilinda miundombinu hiyo kwani inapo haribiwa wao ndio wanaotaabika. 

Amemtaka kila mmoja awe mlinzi wa miundombinu inayogharamiwa na serikali yao
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania