CURRENT NEWS

Friday, May 11, 2018

JAFO-RAIS MAGUFULI ANAWEKA HISTORIA KUBWA KATIKA SEKTA YA AFYA NCHINIWaziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akiweka jiwe la msingi kituo cha Afya Kayanga wilaya ya Karagwe.
 Baadhi ya majengo ya kituo cha Afya Kayanga
 Baadhi ya majengo ya kituo cha Afya Kayanga
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akizungumza baada ya kuweka jiwe la msingi.

Wataalam wa afya kituo cha Afya Kayanga wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo.
.............................................................
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amewaeleza wananchi wa wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera kwamba Rais Dk.John Pombe Magufuli anaweka historia kubwa hapa nchini katika sekta ya afya kwa kuboresha vituo vya afya 208,  ujenzi wa hospitali mpya 67 kwa shilingi Sh.bilion 105  mwaka 2018/2019.

Sambamba hilo, pia ameimarisha bajeti ya dawa kutoka sh.Bilioni 31 mwaka 2015 hadi sh. bilioni 269 kwa mwaka 2017/2018.

Jafo ameyasema hayo leo hii alipokuwa anaweka jiwe la msingi katika kituo cha Afya Kayanga wilayani Karagwe ambacho ni miongoni mwa vituo 208 vinavyo boreshwa hapa nchini.

Jafo amesema " Historia inajengwa kwani tulikuwa tuna vituo vya afya 115 vilivyokuwa na uwezo wa kufanya upasuaji toka Uhuru lakini kwa miaka miwili na nusu ya Rais Magufuli vituo 208 vitaweza kufanya upasuaji na hivyo kuwa na jumla ya vituo 323 vitakavyoweza kufanya upasuaji.

"Pia tulikuwa na hospitali 77 pekee tokea uhuru lakini mwaka huu TAMISEMI tumetenga shilingi  bilion 105 kwa kujenga hospitali mpya za wilaya 67 na karagwe ikiwemo,"amesema.

Katika uwekaji wa jiwe hilo la msingi ulihudhuriwa na mamia ya  Wananchi wa wilaya ya Karagwe licha ya kuwepo na mvua.

 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania