CURRENT NEWS

Tuesday, May 15, 2018

KAMATI YA BUNGE YA UGANDA YAMWAGIA SIFA MRADI DMDP

 Naibu Waziri OR-TAMISEMI Mhe. Josephat Kandege (kushoto) akiwapokea wajumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa toka Nchini Uganda waliotembela Wizara kuona ubora wa miradi ya Benki ya Dunia inavyotekelezwa.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa toka Uganda (PAC-LG) Mhe. Ronald Reagan Okumu (kulia) akiwa na mjumbe wa Kamati hiyo toka Uganda wakifuatilia kikao na Naibu Waziri wa Tamisemi(hayupo pichani) Mhe. Joasephat Kandege.
 Naibu Waziri OR-TAMISEMI Mhe. Josephat Kandege akifurahia jambo wakati wa kikao cha Mapokezi ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa.
Wataalam wanaosimia Miradi ya Benki ya Dunia OR-TAMISEMI pamoja na Kamati ya Bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa toka Uganda wakimskiliza mtaalamu wa maabara ya mradi wa DMDP
Wataalam wanaosimia Miradi ya Benki ya Dunia OR-TAMISEMI pamoja na Kamati ya Bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa toka Uganda wakimskiliza mtaalamu wa maabara ya mradi wa DMDP
....................................................
Kamati ya Bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa kutoka Nchini Uganda (PAC-LG) imemwagia sifa Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es salaam unaoendelea kutekelezwa katika Manispaa ya Tano za Mkoa wa Dar es salaam.

Kamati hiyo yenye zaidi ya wajumbe kumi waliotemebelea Mradi wa DMDP unaotekelezwa chini ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa wamesema ni mradi wa mfano na kuigwa na Nchi za Afrika Masshariki zinazopata mkopo wa fedha kutoka Benki ya Dunia.

Akizungumza katika ziara hiyo ya mafunzo Mwenyekiti wa Kamati hiyo (PAC-LG) Mhe. Ronald Reagan Okumu amesema lengo la ziara yao ni kuona namna ambavyo miradi ya Uboreshaji Miundombinu inayotekelezwa kwa fedha za Mkopo toka Benki ya Dunia;

“Tunapenda kuona ubora wa miradi hiyo, taratibu za ulipaji fidia zilivyofuata, maelekezo ya mkopo wa fedha hizo yalivyozingatiwa na zaidi namna ambavyo fedha zilivyopokelewa, zinavyosimamiwa na wataalamu, zinavyotumika na zinafanyiwa ukaguzi na zaidi suala zima la thamani ya fedha”Value for Money” kuonekana katika miradi hiyo” alisema Mhe. Okumu.

Akipokea ujumbe huo toka Bunge la Uganda Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Josephat Kandege amesema mradi huu umetekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu sasa na mafanikio yaliyopatikana ni makubwa na kwa kiasi kikubwa umesaidia kuwapunguzia kero wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam.

“Karibu mjifunze kwa kuona mtaona barabara zilivyojengwa kwa ubora wa hali ya juu, njia za bora waenda kwa miguu, mifereji yenye viwango ya kusafirishia maji ya mvua, masoko na ofisi za miradi pamoja na maabara za kisasa za kupima ubora wa barabara zinazoendelea kujengwa “ alisema Kandege.

Akielezea Miradi inayotekelezwa chini ya fedha za Mkopo wa Benki ya Dunia Mratibu wa Miradi hiyo toka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Eng. Davis Shemangale amesema kuwa mradi huu unatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano na unalengo  la kuboresha Jiji la Dar es salaam lizidi kuwa bora katika Sekta ya miundombinu, usafiri mjini pamoja na  usalama.

Eng. Shemangale aliongeza  kuwa mradi huo pia utaboresha makazi bora sambamba na kujenga uwezo wa Kitaasisi pamoja na mifumo stahiki na ya kutosha kutunza kumbukumbu na takwimu  itakayosaidia katika Ukusanyaji wa mapato.

Naye mratibu wa mradi wa uendelezaji wa Jiji la Dar es salaam (DMDP) Eng. Emmanuel Ndyamukama amesema Katika awamu ya kwanza ya mradi huu itagharimu jumla ya Dola za Kimarekani Milioni 300 ambazo ni Fedha za Mkopo kutoka Benki ya Dunia. Aidha Shirika la maendeleo la Nchi za Nordic litatoa ruzuku ya dola za kimarekani Mil. Tano kwa ajili ya kukabili changamoto za mabadiliko ya Tabia ya Nchi na huku Serikali ya Tanzania ikichangia takribani Dola za Kimarekani  Mil. 25.3 kwa ajili ya kulipa fidia wananchi  walioathirika na mradi.

Kamati ya Bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa iko katika ziara ya mafunzo kwa muda wa siku Tano na itatemebela miradi ya uendelezaji wa Jiji la Dar es salaam (DMDP), Mabasi yaendayo haraka (BRT) kasha kuelekea katika Manispaa ya Morogoro ambako watatembelea mradi wa uboreshaji na uimarishaji wa Mamlaka za Miji (ULGSP) kasha kumalizia na Jiji la Dodoma ambako watajione mradi wa Uboreshaji Miji Kimkakati (TSCP).

 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania