CURRENT NEWS

Monday, May 14, 2018

KATIBU MKUU WA WIZARA YA ARDHI,NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI AWATAKA WAJUMBE WA BARAZA LA WAFANYAKAZI SHIRIKA LA NYUMBA KUONGEZA TIJA NA KUKIDHI MAHITAJI KWA UMMA

Katibu Mkuu Wa Wizara ya Ardhi Ya ,Nyumba na Maendeleo Ya Makazi.Dorothy Mwanyika Akifungua mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Shirika la Nyumba NHC uliofanyika kwenye makao makuu ya shirika hilo Upanga jijini Dar es salaam wa puli kutoka Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Felx Maagi.

Wajumbe Wa Bazara LA Shirika la Nyumba NHC wakiwa kwenye mkutano huo uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wafanyakzi wa Shirika la Nyumba NHC wakiwa katika mkutano huo.
Wajumbe wa Baraza wakifuatilia mkutano huo.
Wajumbe wa Baraza wakifuatilia mkutano huo.
.................................................................
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi ,nyumba na Maendeleo ya Makazi Dorothy Mwanyika amewataka wajumbe wa Baraza la shirika la nyumba kusimamia masuala muhimu ya kikako hicho ambapo watatoka na mazio yatakayowezesha shirika kuongeza tija na kukidhi Mahitaji kwa umma wa watanzania ambayo kwa sasa yako juu kutokana na imani iliyojengeka.

Ajenda ya kikao hicho zimejielekeza katika masuala ya utendaji wa shirika kupitia mizania ya hesabu za shirika kwa mwaka wa fedha 2018/2019,pamoja na kujadili taaarifa za utekelezaji wa mpangilio unaoendana na mpango mkakati na utaratibu unaoleta mizania ya utekelezaji wa majukumu ya kuimarisha changamoto zinazozikabili shirika hilo.

’’Bazara hili lina jukumu muhimu sana mahala pa kazi kwani ni kiuganishi kati ya menejimeti na Wafanyakazi .Ni Matumaini yangu kuwa mtaendelea kushikiana ili kuleta ufanisi kwa Mamlaka Na Taifa kwa ujumla.’’alisema Katibu Mkuu

Hata hivyo ikumbukwe kuwa Serikali imezitaka tasisi zake kuwa na Mabaraza ya Wafanya kazi Kwani yalianzishwa kwa madhumuni ya kuimarisha Serikali katika ngazi ya kila idara,taasisi na Wizara kuhusu usimamizi wa kazi na rasilimali watu,utekelezaji wa majukumu ,kulinda haki na wajibu wa waajiri na wafanyakazi ikiwa ni pamoja na kutoa ushauri kwa ajili ya kujenga taifa,.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania