CURRENT NEWS

Monday, May 21, 2018

KISARAWE WAMSHUKURU RAIS MAGUFULI

Mkurugenzi wa Dawasa na Mkurugenzi wa kampuni ya CHICO wakisaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji Kisarawe.
Mbunge wa Kisarawe na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akimshukuru Rais Magufuli kwa mradi wa maji Kisarawe.
Viongozi mbalimbali walioshiriki hafla ya utiaji saini utekelezaji wa mradi wa maji Kisarawe.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe akizungumza na wananchi wa Kisarawe.
................................................
Wananchi wa wilaya ya Kisarawe leo wamemshukuru sana Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwasaidia mradi mkubwa maji kutoka chanzo cha Ruvu juu kilichopo maeneo ya Kibamba kuja Kisarawe.

Maji hayo yatasaidia maeneo ya Kisarawe mjini pamoja na maeneo ya visegese ambayo yametengwa kwa ajili ya viwanda.

Shukrani hizo zimetolewa leo wakati wa kusaini  Mkataba wa ujenzi wa mradi huo Kati ya wizara ya maji kupitia kwa mkurugenzi wa DAWASA na kampuni ya CHICO mbele ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Isack Kamwelwe, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo ambaye ni mbunge wa Kisarawe, na Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhe. Ndikilo.

Mradi huo itagharimu shilingi bilioni 10.8 ambapo unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 15.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi hao, Waziri Jafo  amemshukuru sana Rais Magufuli kwa mradi huo mkubwa maji kwani utakuwa mkombozi kwa wakazi wa Mji wa Kisarawe. 

Pia Waziri Jafo amemuomba Waziri Kamwelwe kuangalia uwezekano wa kupeleka maji kutokea Mlandizi kwenda Mzenga na Maneromango.

Pia ameomba kupeleka mashine ya kusimamia maji kijiji cha Gwata

Maombi hayo yamepokelewa vyema na Waziri wa maji na hivyo kuleta matumaini makubwa zaidi kwa wananchi wa wilaya ya Kisarawe. 

Katika hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Pwani Mhe. Zainabu Matitu Vulu, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kisarawe Mhe. Khalfan Sika, pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe Mhe.  Hamis Dikupatile ambao wote kwa pamoja waliungana na Mbunge Jafo kutoa shukran zao kwa Rais Magufuli kwa jambo hilo kubwa la kihistoria.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania