CURRENT NEWS

Monday, May 7, 2018

WAZIRI JAFO:SITAKI UKANJANJA KATIKA UJENZI WA STENDI YA MABASI MBEZI LUIS

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akiwa na Viongozi wa mkoa wa Dar es salaam na wilaya ya Ubungo katika ukaguzi wa eneo la ujenzi wa Stendi ya Mbezi Luis.

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akikagua mipaka ya eneo la ujenzi wa Stendi ya Mbezi Luis.
 Viongozi mbalimbali wakisikiliza maelekezo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo kuhusu ukaguzi wa eneo la ujenzi wa Stendi ya Mbezi Luis.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akipata maelezo ya eneo linalotarajiwa kujengwa stendi ya mabasi ya kisasa ya Mbezi Luis.
............................................................
WAZIRI  wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amewaonya watu ambao ni makanjanja wa miradi ya maendeleo kwamba hatasita kuwachukulia hatua kali za kisheria huku akisema hatarajii kuwaona katika mradi wa stendi ya mabasi ya mikoani inayotarajiwa kujengwa Mbezi Luis jijini Dar es salaam.

Jafo ameyasema hayo alipotembelea eneo linalotarajiwa kujengwa stendi hiyo eneo la Mbezi Luis jiji Dar es salaam. 

Ujenzi wa stendi hiyo unatarajiwa kuanza kujengwa miezi michache ijayo baada ya jiji la Dar es salaam kupata fedha Sh. bilioni 50 kutoka serikali kuu kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati inayotekelezwa chini ya Ofisi ya Rais TAMISEMI. 

Akizungumza katika eneo hilo, Jafo amesema kuna baadhi ya watu wanapoona miradi mikubwa kama hiyo huwa wanapanga mikakati ya kuhujumu au kujipatia fedha kwa kufanya ufisadi.

"Wataofanya hivyo waelewe wazi  hawatabaki salama," Amesisitiza  Waziri Jafo

Aidha, Jafo amesisitiza kauli ya Rais Dk.John Magufuli aliyoitoa wakati akizindua stendi ya mabasi ya Msamvu kwamba katika ujenzi wa stendi zote lazima zizingatie mahitaji ya wadau mbalimbali hususan Mama na baba Nitilie ili waweze kujipatia fedha kutokana na uuzaji wa chakula. 

Naye, Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam  Zipora Liana amemuahidi Waziri Jafo kwamba stendi hiyo itakuwa ya mfano barani Afrika kwani itajengwa kisasa zaidi.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania