CURRENT NEWS

Friday, May 18, 2018

ZIARA YA DC IKUNGI YAVUNA VIONGOZI NA WANACHAMA WA CHADEMA 288.


 Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akizungumza na walimu na wajumbe wa bodi ya shule ya Sekondari ya Mifumbu.
 Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akiwa ziarani katika shule ya sekondari ya Lighwa.
 Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu  akikagua miundombinu ya kuvunia maji ya mvua katika shule ya msingi Mampando.

 Katibu mwenezi wa CCM Wilaya Pius Sankha akiwaongoza wanachama wapya waliotoka Chadema na kujiunga na CCM  kutamka ahadi za mwanachama.
 Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akikagua msingi wa ujenzi wa maabara katika shule ya sekondari ya Lighwa   uliokwama tangu mwaka 2009.
 Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara wa kijiji cha Mampando.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akikagua kiwanja cha michezo cha  Mampando ikiwa ni sehemu ya ziara yake.
......................................................................................................

ZIARA ya mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida Miraji Mtaturu katika kata ya Lighwa na Ntuntu wilayani humo imewarudisha Chama Cha Mapinduzi (CCM)Viongozi  na wanachama 62 wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)miongoni mwao akiwemo katibu wa Baraza la Vijana la Chama hicho(BAVICHA)jimbo la Singida  Mashariki Pascal Jingu.

Mbali na katibu huyo yupo pia katibu wa chadema katika  kata mbili za Ntuntu na Lighwa ambae pia ni mwenyekiti wa kitongoji cha Sanya Mpifi Mussa na wajumbe wawili wa serikali ya kijiji cha Lighwa.

Wakizungumza katika ziara hiyo viongozi hao na wanachama wamesema wameamua kuhama Chadema na kujiunga na CCM ili kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais Dokta John Magufuli na za Mkuu wa Wilaya Ikungi katika kuwaletea maendeleo wananchi.

"Sisi kwa hiyari yetu tumeamua kuhama chama, hatuoni sababu ya kuendelea kuwa katika sehemu ambayo sharti lake ni lazima upinge kila kitu hata kama ni kizuri, sisi sote ni mashahidi tunaona kazi nzuri inayofanywa na viongozi wetu hawa katika kuhakikisha tunapata maendeleo, tuwaunge mkono,"alisema mmoja wao.

Akizungumza katika ziara hiyo Mtaturu amesema serikali imedhamiria kuboresha sekta ya elimu na imekuwa ikitoa fedha za elimu bila ya malipo.

"Katika wilaya yetu ya Ikungi serikali kupitia mamlaka ya elimu Tanzania zimeletwa shilingi milioni 141 kwa ajili ya kujenga nyumba 6 za walimu wa  sekondari ya Lighwa na kila mwezi serikali inaleta zaidi ya sh. Milioni 72 kwa shule za sekondari na msingi,"alisema Mtaturu.

Amesema kutokana na kazi kubwa inayofanywa na serikali wananchi na wadau wana wajibu wa kuunga mkono juhudi hizo za serikali katika uwekezaji wa elimu ikiwemo miundombinu na kuwa na lishe shuleni ili kuongeza ufaulu mashuleni.

"Tunampongeza sana mhe Rais kwa dhamira yake ya kusimamia rasilimali za nchi ambapo kwa kufanya hivyo pesa zinapatikana na  zinaletwa kuwahudumia wananchi kwenye huduma za maji,miundombinu,afya na elimu,"aliongeza mkuu huyo.

Katika ziara hiyo mkuu wa wilaya Mtaturu alitembelea  shule za sekondari Lighwa na Mifumbu zilizopo kata ya Ntuntu na kuchangia tofali 1000,saruji mifuko 20 kwa ajili ya kujenga maabara, bati 30 kwa ajili ya kupaua ofisi ya kijiji na bati 50 kwa ajili ya kupaua madarasa ya  shule ya msingi Sanya.

Aidha alichangia madawati 131 kwa ajili ya shule za msingi Mampando na Mughumbu na bati 100 kwa ajili ya maabara ya Sekondari Ntuntu.

Pia alitoa magoli ya chuma  kwa ajili ya uwanja wa michezo uliopo Mampando na mizinga 20 ya kufugia nyuki kwa vijana wa timu ya Mampando waliokuwa washindi wa kombe la ligi ya Ikungi Elimu 2017.

Ziara hiyo iliyoanzia Kata ya Kikio,Misughaa na baadae Makiungu na Mungaa imewarejesha CCM jumla ya wanachama 288 wa CHADEMA ambapo aliambatana na Katibu Mwenezi wa CCM wilayani humo Pius Sankha.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania