CURRENT NEWS

Saturday, June 9, 2018

CHUO CHA HOMBOLO CHATAKIWA KUJITANGAZA


 Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa mhe. Josephat Sinkamba Kandege akionyeshwa mandhari ya Chuo na Mkuu wa Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Dkt. Madale Rector alipofanya ziara ya kutembelea chuo hicho hivi karibuni.
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa mhe. Josephat Sinkamba Kandege akionyeshwa ukumbi Chuo na Mkuu wa Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Dkt. Madale Rector alipofanya ziara ya kutembelea chuo hicho hivi karibuni.
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa mhe. Josephat Sinkamba Kandege akionyeshwa mandhari ya Chuo na Mkuu wa Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Dkt. Madale Rector alipofanya ziara ya kutembelea chuo hicho hivi karibuni
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa mhe. Josephat Sinkamba Kandege akifafanua jambo kwa Mwenyekiti wa Bodi mpya ya Shirika la Masoko Kariakoo alipokutana nayo wakati wa kikao cha kwanza cha Bodi hiyo baada ya kuchaguliwa lichokuwa kikifanyika katika Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo.

.............................................................
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Josephat Sinkamba Kandege amekitaka chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo kujitangaza hadi nje ya mipaka ya Tanzania ili kiweze kutumika ipasavyo.

Ameyasema hayo hivi karibuni alipotembelea chuo cha Hombolo kuangalia maendeleo ya chuo hicho na kusema kuwa mafunzo yanayotolewa hapo yanalenga kuongeza na kuleta ufanisi katika serikali za mitaa nchini.

Amesema Chuo Kiongozi cha Mafunzo ya Serikali za Mitaa Hombolo kipo mahusisi kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wanaoajiliwa kwenye Serikali za Mitaa  nchini.

“Ni vizuri tukakumbuka kuwa chuo hiki kilianzishwa na serikali kwa lengo la kuwaandaa wafanyakazi wa kada zote katika Serikali za Mitaaa,” alisema na kuongeza kuwa Serikali itaendelea kukijengea uwezo chuo hicho ili kiweze kutoa wahitimu bora.

Mhe Kandege amazitaka Taasisi za Umma na hasa Serikali za Mitaa kuhakikisha wanatumia chuo hicho katika kuwapa watumishi na uongozi stadi za kazi.

Amekipongeza Chuo hicho kwa kutunza mandhari na mazingira mazuri chuo pamoja na miundombinu iliyopo.

Wakati huohuo Mhe. Kandege alipata fursa ya kukutana na Bodi mpya ya Shirika la Masoko Kariakoo ambayo ilikuwa inapata mafunzo hapo kwa siku mbili na kufanya kikao cha kwanza cha Bodi baada ya kuteuliwa.

Akizungumza na Bodi mpya  ya Shirika hilo ameitaka kuhakikisha inatumia  uwezo wake kuongeza wigo wa Shirika la Masoko Kariakoo na kujenga  masoko mengi ndani na nje ya Dar-es-salaam kama ilivyodhumuni la uanzishwaji wa Shirika.

Aidha Ameitaka Bodi hiyo kufuatilia mali zote za shirika na kuhakikisha zinamilikiwa na shirika hilo.

 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania