CURRENT NEWS

Wednesday, June 6, 2018

HALMASHAURI YA WILAYA YA CHEMBA YAFANYA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI


Na Shani Amanzi,

Mkuu wa Wilaya wa Chemba Mhe.Saimon Odunga amewataka Watendaji na Wataalam wa Halmashauri kusimamia Sheria ndogo za katika ngazi za kata na vijiji katika kuendelea kuisimamia ili kuthibiti uharibifu wa mazingira.

Mhe.Saimon Odunga amesema “ikiwa leo ni siku ya Mazingira Duniani na utaratibu huu hufanyika kila mwaka kuanzia tarehe 1mpaka tarehe 6mwezi Juni hufanyika maadhimisho haya, kwa hiyo ni lazima kuzuia viashiria hivyo ikiwemo ukataji wa miti ovyo kwa ajili ya uchomaji mkaa na kuni,uchomaji moto ovyo misitu,utupaji takataka ovyo,kilimo katika maeneo ya miteremko mikali na uchimbaji wa mawe”

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chemba Dkt.Semistatus Mashimba amesema Halmashauri ya Chemba kwa kushirikiana na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) wanaendelea na Kampeni ya kupanda miti ndani ya Wilaya ya Chemba.

“Kwa mwaka huu wa 2018-2019 tunatarajia kupanda miti laki tano ,hii ni utekelezaji wa mpango lioasisiwa na Makam wa Rai,Mhe Samiah Suluhu wa kuufanya Mkoa wa Dodoma kuwa wa kijani sambamba na kuisaidia jamii kupata nishati ya kupikia kama vile kuni”aliongeza kwa kusema hivyo  kt.Mashimba.

Kwa upande wa Mkuu wa Idara wa Usafi na Mazingira wa Halmashauri ya Chemba Ndg.Mohamed Semdoe amesema kwa kushirikiana na Viongozi katika ngazi za Kata na Vijiji ,tunaendelea kushiriki katika zoezi la usafi wa mazingira kila siku ya Jumamosi ya mwisho wa mwezi.

Pia Idara ya Usafi na Mazingira imeanzisha mkakati wa kutenga maeneo ya dampo katika ngazi za vijiji pamoja na kuhamasisha jamii zishiriki katika kuchangia gharama za uzoaji taka kutoka katika maeneo ya makazi na biashara.

Kauli mbiu ya mwaka huu Kitaifa ni “MKAA NI GHARAMA;TUMIA NISHATI MBADALA” ambapo ilikwenda sambamba na uzinduzi wa dampo la Kijiji cha Kidoka ,Kata ya Kidoka, Tarafa ya Goima wilayani Chemba,tarehe 5/6/2018.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania