CURRENT NEWS

Friday, June 8, 2018

MASHINDANO YA UMISSETA YAENDELEA JIJINI MWANZA
Na Mathew Kwembe, Mwanza
Mashindano ya UMISSETA yanayoendelea katika viwanja vya Chuo cha Ualimu Butimba na Shule ya Sekondari Nsumba yanatarajiwa kufunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa mnamo tarehe 9 juni 2018 katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Hadi kufikia jana mashindano hayo yameshuhudia michezo mbalimbali ikichezwa katika viwanja vya Nsumba na Butimba ambapo jumla ya mikoa 28 inashiriki mashindano hayo
Kwa mujibu wa matokeo yaliyotolewa na Mratibu wa mashindano hayo bwana Leonard Tadeo, katika mchezo wa mpira wa miguu wavulana, timu za Kilimanjaro na Mbeya zilitoka sare kwa kufungana goli 1 kwa 1 huku Ruvuma wakiifunga Kigoma 2-1.
Matokeo mengine yanaonyesha kuwa Geita waliifunga Dar es salaam 1-0, Shinyanga 1 na Simiyu 1, Singida 2 na Dodoma 1, Tanga 1 Pemba 0, Iringa 1 na Katavi 1, Rukwa 0 na Arusha 0, Mwanza 3 na Tabora 0, Unguja 2 na Njombe 0, Morogoro 1 Mara 0, na Manyara 0 Mtwara 0.

Kwa upande wa mpira wa miguu wasichana matokeo yanaonyesha Mbeya 3 Lindi 0, Ruvuma 1 Kilimanjaro 1, Dar es salaam 4 Geita 0, Simiyu 2 Shinyanga 1, Singida 1 Mara 1, Arusha 2 Iringa 1, Mwanza 2 Katavi 1na Morogoro 3 Njombe 2.
Matokeo ya Netiboli yanayonyesha wasichana Shinyanga 23 Tanga 15, Mara 31 Njombe 15, Dar es Salaam 55 Kilimanjaro 8, Dodoma 29 Simiyu 17, Morogoro 45 Kagera 13, Geita 31 Ruvuma 27, Manyara 19 Mtwara 17, Mbeya 25 Kigoma 20, Mwanza 44 katavi 19, Arusha 28 Rukwa 23,
Kwa upande wa mpira wa kikapu wasichana, Morogoro iliibugiza Manyara kwa vikapu 106 kwa vikapu 16. Matokeo mengine yanaonyesha Kigoma 48 Geita 31, Mtwara 35 Mara 19, Mwanza 31 Arusha 16,  na Iringa 20 Arusha 17.
Katika mchezo wa mpira wa kikapu wavulana matokeo yanaonyesha kuwa Kilimanjaro 26 Dar es salaam 15, Dodoma 34 Shinyanga 24, Tanga 40 Pemba 28, Unguja 62 Njombe 13, Mara 43 Kagera 11, Mbeya 68 Lindi 11, Dodoma 53 Pemba 23, Dar es salaam 32 Kigoma 15, Tanga 55 Songwe 10, Katavi 69 Tabora 13, Pwani 101 Rukwa 14, na Arusha 40 Iringa 37.
Matokeo ya mpira wa wavu wavulana yanaonyesha kuwa Manyara imeifunga Unguja kwa seti 3- 2. Matokeo mengine yanaonyesha Morogoro 3 Kagera 0, Mtwara 3 Njombe 1, Shinyanga 3 Dodoma 0, Dar es salaam 3 Kigoma 0, Tanga 3 Songwe 0, Mbeo 3 Lindi 0, Singida 3 Pemba 0, Manyara 3 Njombe 0, Mara 3 Kagera 0, Arusha 3 Iringa 1 Mwanza 3 Katavi 0 na Pwani 3 Tabora 1.

Mpira wa wavu wasichana matokeo yanaonyesha Manyara 3 Kagera 0, Simiyu 3 Dodoma 1, Tanga 3 Songwe 0, Mbeya 3 Lindi 2, Singida 3 Simiyu 0, Iringa 3 Tabora 0 na Mwanza 3 Arusha 1.
Kwa upande wa mpira wa mikono wasichana katika michezo iliyochezwa jana matokeo ni Mtwara 12 Kagera 8, Songwe 20 Tanga 8, Mbeya 11 Lindi 8, Dar es salaam 13 Kilimanjaro 8. Njombe 5 Manyara 5, Tabora 7 Iringa 3, Katavi 11 Rukwa 6 na Mwanza 16 Iringa 13.
Mpira wa mikono wavulana matokeo ni Dar es salaam 26 Kilimanjaro 7, Songwe 23 Dodoma 18, Kilimanjaro 15 Ruvuma 9, Singida 17 Songwe 14, Unguja 25 Njombe 17, Mara 20 Kigoma 12, Dodoma 16 Simiyu 1, Kigoma 25 Geita 13, Rukwa 17 Pwani 16, Mwanza 19 Katavi 12, na Arusha 23 Iringa 15

 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania