CURRENT NEWS

Friday, June 8, 2018

MIKOA YA IRINGA NA KAGERA YATAMBA FAINALI RIADHA MAALUMMwanariadha Shija Italange kutoka mkoa wa Pwani ambaye alishika nafasi ya kwanza katika hatua ya nusu fainali akikimbia katika mbio za mita 400 katika viwanja vya Butimba jijini Mwanza jana.


Mwanariadha Epimarki Bonifasi kutoka shule ya Sekondari Makongo akiwakilisha mkoa wa Dar es salaam katika mbio za mita 1500 ambapo alishika nafasi ya kwanza hatua ya fainali.Winfrida Makenzi kutoka mkoa wa Dar es salaam akimalizia mbio fupi za mita 100 hatua ya nusu fainali na kuwa wa kwanza.
....................................................
Na Mathew Kwembe, Mwanza
Washiriki wa mchezo wa riadha maalum kwa mbio fupi kutoka mikoa ya Iringa na Kagera wametamba katika mashindano ya UMISSETA yaliyofanyika jana katika viwanja vya Butimba baada ya kushika nafasi tatu za juu kutoka mikoa hiyo.
Katika mchezo wa riadha maalum hatua ya fainali kwa mbio fupi za mita 100, washiriki wawili kutoka mkoani Iringa ambao ni Mathias Peter aliyetumia sekunde 12: 72 na Sudy Bakari aliyetumia sekunde 13:20 ambao kwa pamoja waliibuka kidedea kwa kushika nafasi ya kwanza na ya tatu.
 Nafasi ya pili ilishikwa na Fred Wangabu kutoka mkoani Rukwa ambaye alitumia sekunde 13:16.
Washindi wengine ni pamoja na Yusuph Samwel kutoka mkoani Dodoma aliyeshika nafasi ya nne, Yumen Ezekiel pia kutoka Dodoma ambaye alishika nafasi ya tano, Mohamed Hussein kutoka Kilimanjaro alishika nafasi ya sita na Martin Frank Kibwe kutoka mkoani Rukwa ambaye alishika nafasi ya saba.
Kwa upande wa riadha maalum mbio fupi wasichana nafasi ya kwanza ilishikwa na Kelen Silvester kutoka mkoani Kagera aliyetumia sekunde 18:22 na Anifa Damian pia kutoka Kagera aliyetumia sekunde 18:50 huku nafasi ya tatu ikishikwa na Olive Cyprian kutoka mkoani Kilimanjaro ambaye alitumia sekunde 22:13
Mbali na riadha maalum, pia kulifanyika mashindano ya mchezo wa riadha hatua ya nusu fainali kwa wavulana na wasichana.


 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania