CURRENT NEWS

Monday, June 4, 2018

DK.KAPOLOGWE ARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA VITUO VYA AFYA NCHINI

Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe , Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dr. Ntuli Kapologwe akikagua moja ya jengo la  upasuaji  leo katika ziara ya ukaguzi wa mendeleo ya ujenzi katika kituo cha afya cha Mudemu kilichopo katika  Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Jijini Dodoma.
Jengo la Upasuaji lilojengwa katika kituo cha Afya cha Mundemu katika kituo cha afya cha Mudemu kilichopo katika  Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Jijini Dodoma.

 Timu ya Dodoma ikikagua baadhi ya miundombinu ya kituo cha afya cha Mudemu kilichopo katika  Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Jijini Dodoma wakati wa ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho.

Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe , Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dr. Ntuli Kapologwe akikagua ramani inayoonyesha jengo la wazazi katika kituo cha afya cha Mudemu kilichopo katika  Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Jijini Dodoma.
...............................................
Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe , Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dr. Ntuli Kapologwe amesema kuwa ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa vituo vya afya nchini  ambavyo vimejengwa  kwa ushirikiano baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wafadhili mbalimbali wa Sekta ya afya nchini.

Ameyasema hayo leo wakati alipotembelea kituo cha afya Mundemu kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Jiji la Dodoma kuona maendeleo ya ujenzi wa vituo vya afya nchini na kujionea matumizi ya fedha ambazo zimetolewa na Serikali katika awamu ya tatu ambayo ni ya kukarabati vituo 39.

Dr. Kapologwe amesema Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR-TAMISEMI) tayari imeshaagiza vifaa tiba ambavyo vitawekwa katika majengo hayo na imeweza kuajiri watumishi wapatao 6180 ambao watapelekwa katika vituo vyote vya afya viliyoojengwa nchini ili waweze kuanza kutoa huduma kwa jamii.

Amesema vituo hivyo vitaweza kutoa huduma ya upasuaji, pamoja na huduma nyingine za wagonjwa hivyo watumishi wapya watakuwa wakitoa huduma bora kwa wananchi lengo likiwa ni kutoa huduma bora za afya na kupunguza malalamiko kwa wananchi kuhusu huduma za afya nchini.

Anaendelea kufafanua kuwa upangaji wa watumishi hao katika vituo vya afya utakuwa wa kimkakati kwa maana ya kwamba tayari wameshaainisha mahitaji na watapangiwa vituo vya kazi kulingana na mahitaji ya eneo husika ambapo kutaondoa changamoto ya upungufu wa watumishi wa afya nchini.

Wakati huohuo, Mkurugenzi wa Idara ya Tawala za Mikoa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa  na Serikali za Mitaa Bi. Beatrice Kimoleta ameridhishwa na ujenzi wa vituo vya afya nchini na kuwataka baadhi ya maeneo kuongeza kasi ya ujenzi ili kukamilisha vituo hivyo kwa wakati
Amesema kuwa katika Ujenzi wa vituo vya afya nchini umeweza kuzingatia dhamani ya fedha iliyotolewa na Serikali  ukilinganisha na majengo yanayojengwa ambayo ni imara na amewapongeza Kamati ya Ujenzi ya Kituo cha afya cha Mpwayungu kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa kituo hicho.

Aidha Bi. Kimoleta  ameushauri uongozi wa jiji la Dodoma kuhakikisha wanamaliza ujenzi wa Kituo cha afya cha Mpwayungu kwa  wakati lakini kwa kuzingatia ubora wa majengo ili wananchi waweze kupata huduma za afya katika eneo hilo.

 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania