CURRENT NEWS

Wednesday, June 6, 2018

WAJASIRIAMALI WA WILAYA YA CHEMBA WAPATA MAFUNZO YA UJASIRIMALI


 Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Saimon Odunga akizindua Mafunzo ya Ujasiriamali yaliofanyika ndani ya siku mbili kuanzia tarehe 5- 6/6/2018 kwa kina mama kupitia Taasisi ya Ulingo kutoka Dar-es-salaam
 washiriki wa mafunzo
 washiriki wa mafunzo
Mratibu wa Taasisi isiyo ya Kiserikali Bi.Saum Rashid akiwataka Wanawake walio pembezoni kujitambua na kuweza kuwa na uwezo zaidi katika ngazi za Uongozi pamoja na Ujasirimali


..............................................................................................................
Na Shani Amanzi,

Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Saimon Odunga amewataka Wanawake washiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi kwani sehemu kubwa ya Viwanda vidogovidogo vinaajiri wakina mama hasa Viwanda vya shughuli za mikono.

Mhe.Saimon Odunga amesema “ shughuli ndogondogo zinakupa faida kubwa tu hasa ukiwa mbunifu
mzuri na Serikali ya Awamu ya Tano ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mhe.Rais John Pombe Magufuli inaendelea kuwapa kipaumbele wakina mama na Vijana kwa kuwapa mitaji na kwa hapa Chemba Serikali yetu inaendelea kuangalia ni namna gani wanaweza kuzidi kuwasaidia wakinamama.”

Aidha Odunga amesema ni vyema kutumia muda wao kujifunza zaidi juu ya ujasirimali kwani shughuli ndogondogo za ujasirimali zinakupa faida kubwa tu hasa ukiwa mbunifu mzuri na kwa Wilaya ya Chemba,wageni wanakaribishwa kutoa mafunzo kwa kina mama ili waweze kuleta maendeleo Chemba.

Naye Mratibu wa Taasisi isiyo ya Kiserikali iitwayo Ulingo, Bi.Saum Rashidi amesema lengo la kuja
Chemba ni kuwafikia wanawake walioko pembezoni kuwawezesha katika Mafunzo ya Uongozi Jinsia na Ujasirimali ili wanapokuwa Viongozi waweze kumudu majukumu yao kama Wanawake Viongozi na wawe mfano wa kuigwa ndani ya jamii husika.

Taasisi hiyo ipo Dar-es-salaam ni Jumuiya ya Wanawake, wanatoa Mafunzo kwa Wanawake wote bila kujali itikadi za Vyama na Mafunzo hayo ya Ujasirimali yamefanyika ndani ya siku mbili kuanzia tarehe 5/6/2018 mpaka tarehe6 /6/2018 katika Ukumbi wa Godown, Chemba.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania