CURRENT NEWS

Friday, June 8, 2018

WANAWAKE WASHIRIKI KUJENGA WODI YA MAMA NA MTOTO CHEMBA

Jengo la Mama na Mtoto liliojengwa katika Kituo cha afya cha Hamai, kilichopo katika Kata ya Songolo, Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma.
Timu ya ufuatiliaji na ukarabari wa vituo vya afya nchini kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, ikiongozwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Charles Kiologwe wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Bw.Jofrey Shima walipotembelea Kituo cha afya cha Hamai, kilichopo katika Kata ya Songolo Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Charles Kiologwe  akitoa maelekezo kwa uongozi wa Halmashauri ya  Wilaya ya Chemba wakati wa ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa kituo cha afya cha Hamai kilichopo katika Wilaya ya Chemba, Mkoani Dodoma.
Timu ya ufuatiliaji na ukarabari wa vituo vya afya nchini kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, ikiongozwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Charles Kiologwe  wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Bw.Jofrey Shima wakati walipotembelea Kituo cha afya cha Hamai, kilichopo katika Kata ya Songolo Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma.

........................................................
Wanawake washiriki kujenga Wodi ya mama na mtoto - Chemba
Wanawake wa Kata ya Songolo, katika Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma wamejitoa katika ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto lililojengwa katika kituo cha afya cha Hamai kilichopo katika Wilaya hiyo kwa lengo la kuchangia nguvukazi ili kupunguza changamoto za kutembea muda mrefu kutafuta huduma za afya.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi  wa kituo hicho Bw. Saidi Msigwa mbele ya timu ya ukaguzi wa ujenzi wa vituo vya afya  katika Mkoa wa Dodoma walipokuwa wakikagua maendeleo ya ujenzi wa vituo vya afya mkoani Dodoma.

Amesema kuwa asilimia kubwa ya wanawake wa Kata ya Songolo walijitokeza katika ujenzi wa kituo hicho kwa kuwa ndicho kilikuwa kilio chao cha muda mrefu cha kujengewa Wodi ya mama na Mtoto jambo lililopelekea wanawake wengi hasa wajawazito kwenda kujifungulia katika Hospitali ya Wialaya ya Kondoa.

Amesema kukamilika kwa Kituo cha afya cha Hamai kutasaidia wananchi wengi kupata huduma ya afya  hasa vijiji vya jirani ambavyo ni  Murongia, Itolwa , Jangalo, Jinjo, Kinkima na Kirerechangombena ambao wote hupata huduma katika kituo hicho.

Bw. Msigwa amesema mwaka 2015 wanawake wa Kata ya Songolo waliamua kijutolea kujenga jengo la Wodi ya Mama na mtoto kutokana na kuwepo kwa jengo moja la wodi ya Mama na Mtoto jambo ambalo lilikuwa likisababisha msongamano wa wamama wajawazito sababu hii ilipelekea wanawake kuamua kuchimba msingi na kukusanya mawe kwa ajili ya ujenzi wa  wodi hiyo ndipo serikali ilipoamua kujenga jengo hilo mwaka 2018.

Bw. Msigwa ameishukuru serikali kwa kuona umuhimu wa kujenga kituo cha afya cha Hamai ambacho kitasaidia wananchi maskini ambao walikuwa wakitembea umbali mrefu kwenda kutafuta huduma za afya katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa.

Amesema kituo hicho kimejengewa wodi ya mama na mtoto, jengo la upasuaji, maabara, chumba cha kuhifadhia maiti na nyumba ya mtumishi ambapo mpaka sasa tayari zimetumika zaidi ya shilingi milioni 291.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Charles Kiologwe ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya chemba kwa usimamizi mzuri wa majengo yaliyojengwa ambayo yanaonyesha uhalisia wa matumizi ya fedha zilizotumika ukilinganisha na ubora wa majengo.
Aidha ameutaka uongozi wahuo kukamilisha ujenzi huo kwa wakati ili wananchi waweze kupata huduma za afya katika maeneo ya karibu na wanapoishi.

Naye Bi Martha Mariki Afisa afya Mkuu kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ameutaka uongozi wa Halamashauri ya Wilaya ya Chemba kuhakikisha maeneo ya taasisi yanapimwa na kuwa na hati miliki, pia kuhakikisha wanaweka kwenye bajeti kama kipaombele cha kuweka uzio wa maeneo ya taasisi ili kuepusha  maeneo mengi kuvamiwa na wananchi.

 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania