Mtafiti mkuu wa mradi ambao unatoa nafasi ya kufundisha watoa huduma za Afya kuweza kuongeza uwelewa na kupunguza vifo visivyo vya lazima kwa wajawazito na watoto Dk Angelo Nyamtema akiohojiwa na waandishi wa habari ambao hawapo pichani.
Mganga Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro Dk Frenk Jacob akiteta jambo na Mtafiti mkuu wa mradi Dk Angelo
Nyamtema ,anaefatia ni Dr Abdallah Abdallah anetabasamu ni Dakari bingwa wa magonjwa ya akinamama na
uzazi Dk Hassan Njete na wa mwisho ni Dk Sister Nathalia Makunja ambae ni
Daktari Bingwa wa magonjwa ya akinamama na uzazi kutoka katika HospitaI ya mtakatifu Fransisko Ifakara.
......................................................
Watoa huduma
wa afya wametakiwa kufanya kazi kwa ufanisi ili kuepukan na vifo vya akina mama
wajawazito na watoto wachanga ili kuhakikisha takwimu za vifo vya akina mama
wajawazito haziongezeki kama ilivyo sasa
kwani takwimu zinaonyesha vifo vya akina mama vimeongezaka kutoka 454
katika vizazi hai laki moja kwa mwaka
jana hadi kufikia vifo 556 kwenye vizazi
hai laki moja.
Rai hiyo
imetolewa na mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk, Frank Jacob katika mkutano wa
kuwajengea uwezo watoa huduma za Afya kutoka
Zahanati na Vituo vya Afya 20 Mkoani Morogoro
ambapo amesema ili kupunguza vifo vya akina mama wajawazito nilazima wataalamu wa Afya wafate vigezo vya
utoaji wa huduma bora kama kuangalia madhurio ya akima mama Clinic, kutoa dozi
ya pili (ASP) ya kukinga Maralia , Madini ya chuma na Folic Acid kwa mjamzito pamoja na kutoa elimu kuhusu uzazi wa mpango
ambao pia hupunguza vifo vya akina mama kwa asilimia 44.
Post a Comment