CURRENT NEWS

Thursday, June 7, 2018

WATU WATATU KWENDA URUSI KWENYE KOMBE LA DUNIA 2018 KUPITIA PROMOSHENI YA BIA YA KILIMANJARO LAGER


Meneja wa Mawasiliano ya wateja wa TBL, David Tarimo akitoa ufafanuzi wa promosheni ya Kilimanjaro kwa waandishi wa habari,kulia ni Afisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha,Hamidu Semvua na Raj Chandarana aliyeko kwenye mafunzo chini ya mpango wa Global Management Trainee katika kampuni ya TBL.
Meneja wa Mawasiliano ya wateja wa TBL, David Tarimo na Raj Chandarana kutoka TBL wakijadiliana jambo.
Zoezi la droo ya kupata washindi ikifanyika kupitia teknolojia za kisasa.
Meneja wa Mawasiliano ya wateja wa TBL, David Tarimo akiongea kwa simu na mmoja wa washindi wa droo kupitia promosheni ya bia ya Kilimanjaro.
Na Mwandishi Wetu.
Wakazi wawili wa jijini Dar es Salaam na mmoja wa mkoa wa Geita wameibuka wamejishindia tiketi na kugharamiwa safari ya kwenda, Urusi, kuona michuano ya Kombe la Dunia, mubashara kupitia promosheni inayoendelea ya bia rasmi ya Tanzania, katika msimu huu wa Kombe la Dunia ya Kilimanjaro Lager. Droo ya kuwapata washindi hao imefanyika jijini Dar e Salaam, chini ya usimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha ya Taifa na kushuhudiwa na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari.

 Washindi katika droo hiyo wametajwa kuwa ni Charles John (Geita), Kaijage Kironde (Dar es Salaam) na Leodgard Isaac (Dar es Salaam). Washindi hao walipokea habari hizo kwa furaha baada ya kupigiwa na Meneja wa Mawasiliano ya wateja wa TBL, David Tarimo,ambapo walieleza kuwa wanaisubiri safari yao kwa shauku kubwa na kuwataka wateja kuendelea kuchangamkia promosheni hiyo ambayo ilizinduliwa mapema mwezi uliopita. Promosheni hiyo inaenda sambamba na kujishindia muda wa maongezi 2,500/= kila wanaponunua bia ya Kilimanjaro na kushiriki mara (sita) 6 kutuma number iliyopo chini ya kizibo kwenda 15451 fedha taslimu kiasi cha shilingi 1,000,000/- Kila wiki kwa wiki kumi. 

Meneja wa Mawasiliano ya Wateja wa TBL, David Tarimo, alisema, washindi wapatao 10 watawezeshwa kugharamiwa kuona mashindano ya kombe la Dunia na washindi wengi wataweza kujishindia fedha taslimu, na muda wa maongezi. “Lengo kubwa la promosheni hii ni kuwazawadia wateja wetu ili waburudike katika msimu huu wa shamrashamra za kombe la dunia la FIFA 2018”, alisisitiza. Ili kujishindia zawadi mteja anapaswa kutuma namba zilizopo kwenye chupa za bia ya Kilimanjaro kwenda namba 15451 ili kujipatia fedha taslimu na muda wa maongezi, zawadi ya tiketi ni kwa wale wataoshiriki kujibu maswali yatakayoendeshwa kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya www.Kililager.com na kujipatia pointi za ushindi. 

Promosheni hii itadumu kwa muda wa miezi miwili na nusu na itaendeshwa nchi nzima na matangazo yake yanaendelea kutangazwa rasmi kupitia televisheni, radio na mitandao ya kijamii.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania